Sunday, March 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Chama cha ACT-Wazalendo kinawapiga msasa wabunge wake

by TNC
January 12, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Dar es Salaam. Chama cha ACT–Wazalendo kimewapiga msasa wabunge wake wapya ili kujiandaa kutekeleza majukumu yao ya kuisimamia Serikali katika Bunge la Tanzania.

Katika Bunge hilo la 13, linalotawaliwa na uwingi wa wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ACT–Wazalendo itawakilishwa na wabunge wanane, kati ya wabunge 11 wa Vyama vya upinzani huku wanaobakia wakitoka Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma).

Vikao rasmi vya Bunge hilo, vitaanza Januari 27, 2026, ingawa vikao vya kamati za kudumu vimepangwa kuanza Jumanne na kuendelea hadi Januari 26.

Pamoja na mambo mengine, vikao vitakavyoanza, wabunge watajua kamati zao za kudumu, kuchagua wenyeviti na makamu wao na kuelezwa majukumu yao.

TNC imebaini kwamba kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe ameshiriki na kutoa mafunzo maalumu kwa wabunge hao.

Naibu Katibu Idara ya Haki za Binadamu na Vyombo vya Uwakilishi wa Wananchi, Mbarala Maharagande, amesema chama kimetoa mafunzo kwa wabunge wanaotokana na chama chetu, ACT Wazalendo ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kibunge, kwa ufanisi.

Maharagande amesema mafunzo hayo yamehudhuriwa na wabunge wote wa chama jijini Dodoma, yakiwa na lengo la kubadilishana uzoefu na namna ya kuisimamia ipasavyo Serikali, kuwawakilisha wananchi na kutunga sheria ikiwa ndio wajibu wa msingi kwa wabunge.

Akizungumza katika mkutano huo, Zitto ameeleza uzoefu wake wa siasa za kibunge katika kuleta ufanisi na matokeo chanya kwa masilahi ya Taifa, ya chama na wananchi jimboni kwa Mbunge husika.

Maharagande amesema kutokana na mafunzo hayo wabunge anaamini wapo tayari kutekeleza majukumu yao ya Kibunge na kuiwajibisha Serikali kwa masilahi mapana ya Taifa.

"ACT Wazalendo itaendelea na wajibu wake wa msingi wa kuwasemea na kupigania ustawi mwema wa Taifa letu kwa kuhakikisha nchi yetu inaheshimu na kuwa na utawala wa sheria, demokrasia, na kulinda misingi ya haki za binadamu," amesema Maharagande.

Tags: ACTWazalendochaChamakinawapigamsasaWabungewake
TNC

TNC

Next Post

Majeshi yalivyoadhimisha kilele cha miaka 62 ya Mapinduzi

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company