Sunday, March 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Anapa kuzalisha mazao mapya ya utalii

by TNC
January 11, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Hifadhi ya Taifa ya Arusha Yatangaza Mazao Mapya ya Utalii Baada ya Kutambuliwa Kimataifa

Arusha – Baada ya kutambuliwa kimataifa miongoni mwa maeneo bora ya kusafiri mwaka 2026, Hifadhi ya Taifa ya Arusha (Anapa) imejipanga kuanzisha mazao mapya ya utalii ili kuvutia watalii zaidi wa ndani na nje.

Lengo la uanzishaji wa mazao mapya ya utalii ni kuongeza watalii wa nje na ndani ili kujionea vivutio hivyo ikiwemo Mlima Meru, Ziwa Momella na utalii wa kutazama twiga.

Mkuu wa Hifadhi hiyo, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Uhifadhi, Witness Shoo, amesema hayo leo Jumapili Januari 11, 2026, wakati shughuli mbalimbali za utalii zikiendelea hifadhini humo. Ameeleza kuwa utambuzi huo ni heshima kubwa kwa hifadhi hiyo na utawaongezea kupata watalii zaidi.

Shoo amesema kuwa hifadhi hiyo yenye vivutio mbalimbali ikiwemo Mlima Meru, misitu minene, maporomoko ya maji na vivutio vingine, watazalisha mazao mapya ya utalii ili kuongeza watalii wa ndani na nje.

"Hivi karibuni Arusha ilitambuliwa kama sehemu nzuri ya kutembelea ikiwemo Hifadhi ya Arusha, kutokana na vivutio mbalimbali ikiwemo Mlima Meru, kreta ya Ngurdoto na maziwa ya Momella ambayo yanapambwa na ndege aina ya flamingo sambamba na Mto Ngarenanyuki wenye maji ya kahawia na ya kipekee," amesema.

"Tuna misitu minene ambayo ina mbega weupe na weusi ambao unaweza kupiga nao picha kwa karibu lakini kufanya matembezi ya miguu, baisikeli na kupiga makasia ziwani," ameongeza.

Mhifadhi huyo amesema kuwa wataanzisha mazao mapya ya utalii ili kuvutia utalii zaidi pamoja na kuongeza fursa za uwekezaji ambapo waliwakaribisha wawekezaji wa ndani na nje kuchangamkia fursa hizo kwa mujibu wa taratibu na sheria.

"Niwakaribishe kwenye hifadhi ya kipeke ambayo ina mlima, sehemu tambarare, maporomoko ya maji na vitu vingine. Tunahamasisha Watanzania kuendelea kutembelea vivutio vilivyopo nchini," amesema.

Mhifadhi huyo amesema katika kipindi cha mwaka 2024/25 hifadhi hiyo ilikuwa na ongezeko la wageni kutoka 60,000 hadi 72,000 na kuwa wanatarajia mwaka huu kupokea wageni zaidi ya 100,000.

Watalii Washerehekea Uzuri wa Hifadhi

Mmoja wa watalii, Suraji Navarante, amesema kati ya vitu vilivyomvutia hifadhini humo ni pamoja na mwonekano wa Mlima Meru, maporomoko ya maji pamoja na mazingira tulivu.

"Iwapo unataka kufanya safari nimeona hifadhi hii ni miongoni mwa bora kwani kuna mazingira tulivu ambayo yanaweza kufanya safari yako iwe nzuri," amesema.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Emmanuel Buhohela amesema mbali na wageni wa nje, uhamasishaji wa utalii wa ndani umeongeza idadi ya Watanzania kutembelea Hifadhi mbalimbali hapa nchini.

"Uhamasishaji wa utalii umesaidia kwa kiwango kikubwa kuitangaza Tanzania nje pamoja na kuhamasisha utalii wa ndani na tunaendelea kuhamasisha zaidi ili tuongeze mapato," amesema.

Mmoja wa watalii kutoka mkoani Kilimanjaro, Gedion Swai amesema wao kupitia kikundi chao kwa mwaka huu wameamua kutembelea hifadhi huo ili kujionea vivutio vilivyomo.

"Tumeamua mwaka huu tusiingie kuona wageni wakija kwenye hifadhi zetu bali na sisi tuje kujionea vivutio vilivyopo hifadhini na kufurahia kwa pamoja badala ya kuishia mijini tu," amesema.

Hifadhi ya Taifa ya Arusha ilitambuliwa kimataifa Desemba 31, 2025 kama moja ya maeneo bora ya kusafiri kwa mwaka 2026.

Tags: Anapakuzalishamapyamazaoutalii
TNC

TNC

Next Post

Tough task awaits new Home Affairs Minister Katambi

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company