Tuesday, March 17, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Rais aunda tume kutathmini fidia miradi maendeleo

by TNC
December 31, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Rais Mwinyi Aunda Tume ya Kupitia Fidia za Miradi ya Serikali Zanzibar

Unguja – Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ameunda tume ya kupitia na kutathmini masuala ya fidia yanayotokana na utekelezaji wa miradi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Unguja na Pemba.

Hatua hiyo inakuja kufuatia kuibuka kwa malalamiko ya wananchi katika maeneo yanakotekelezwa miradi hiyo ya maendeleo, wakidai kulipwa fedha ndogo isiyoendana na thamani ya mali zao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Desemba 31, 2025, Rais Mwinyi ameteua tume ya wataalamu wanane kutoka taasisi za Serikali na sekta binafsi kufanya kazi hiyo.

Wajumbe wa Tume

Wajumbe wa tume ni Salum Othman Simba ambaye ni mstaafu na mtaalamu wa masuala ya uthamini, Mussa Kombo Mrisho (mwanasheria kutoka Ofisi ya Rais Ikulu), Khamis Muhidini Bakari (mhandisi kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege) na Fauzia Sindi Hassan (Msajili wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi).

Wengine ni Sabrina Yussuf Hassan ambaye ni mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kutoka Ofisi ya Rais Ikulu, Mwanaidi Suleiman Ali (mtaalamu wa masuala ya jamii) kutoka Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi (Zaeca), Ramadhani Nassoro Mwinyi (mtaalamu wa fedha) kutoka sekta binafsi na Mzee Abdallah Khatib (mtaalamu wa umma) kutoka sekta binafsi.

Ushirikiano wa Wananchi Unahitajika

Wananchi wanaombwa kutoa ushirikiano kwa tume hiyo itakapofika katika maeneo husika, kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake.

Wakizungumza kuhusu kuundwa kwa tume hiyo, baadhi ya wananchi wa Kwerekwe wamesema wana matumaini kuwa itatoa suluhu ya kudumu.

"Tathmini inayofanywa inachanganya, wengine wanalipwa fedha nyingi na wengine wanapunjwa. Tunaamini tume hii itakuja na majibu mazuri, tunapongeza hatua hii," amesema Rajab Hassan.

Utekelezaji wa Ahadi za Kampeni

Kuundwa kwa tume hiyo ni utekelezaji wa ahadi aliyotoa Dk Mwinyi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025, alipokutana na makundi mbalimbali ya wananchi.

Moja ya kero iliyowasilishwa na wananchi kwake, ilikuwa madai ya kudhulumiwa malipo ya fidia. Kero hiyo ilijitokeza zaidi katika maeneo ya Fumba, Nyamanzia na Dimani.

Wakati akijibu hoja hizo, Dk Mwinyi alikiri kuwepo kwa changamoto katika baadhi ya tathmini na kuwaahidi wananchi kuunda tume maalumu endapo angerudi madarakani.

Changamoto za Fidia

Rais Mwinyi aliwahi kufafanua kuwa, wakati mwingine baadhi ya wananchi huendeleza maeneo yasiyoruhusiwa kisheria, hali inayosababisha gharama za fidia kuwa kubwa kuliko gharama za mradi wenyewe.

"Wananchi ni muhimu kwa maendeleo, lakini pia miradi lazima itekelezwe kwa sababu bila miradi hatuwezi kupiga hatua za maendeleo," alisema Dk Mwinyi.

Malalamiko ya fidia pia yaliibuka katika mradi wa ujenzi wa barabara za mjini unaohusisha madaraja mawili ya juu ya Amani na Kwerekwe, baadhi ya wananchi walilalamikia fidia ndogo na kutishia kugoma kuondoka katika maeneo yao.

Tathmini Upya ya Fidia

Kwa mujibu wa maelezo ya Serikali, tathmini ya awali haikuhusisha thamani ya ardhi, jambo lililosababisha baadhi ya wananchi kulipwa fidia ndogo.

Baadaye, Dk Mwinyi alisema Serikali iliamua kutafuta kampuni binafsi kufanya tathmini mpya baada ya kubaini changamoto kwa mthamini wa Serikali.

Tags: AundafidiaKutathminimaendeleomiradiRaisTume
TNC

TNC

Next Post

Surge in online scams sparks awareness drive

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company