Sunday, March 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Waathirika wa ajali ya helikopta Mlima Kilimanjaro wametambuliwa

by TNC
December 25, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Ajali ya Helikopta Mlima Kilimanjaro: Miili ya Watu Watano Yatambulika

Moshi – Miili ya watu watano waliofariki kwa ajali ya helikopta ya kampuni ya uokoaji ya Kilimedair meneo ya kati ya Kibo na Barafu Camp, Mlima Kilimanjaro, imetambuliwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, ajali hiyo imetokea Desemba 24, 2025 saa 11:30 jioni wakati helikopta hiyo ikitoka kuchukua wagonjwa Mlima Kilimanjaro.

Kamanda Maigwa amesema helikopta hiyo ilikuwa na watu watano ambao ni Constantine Mazonde raia wa Zimbabwe ambaye alikuwa rubani, Jimy Daniel aliyekuwa daktari na Innocent Mbaga ambaye ni muongoza watalii.

Wengine waliofariki ni Plos David na Plosova Anna ambao wote ni raia wa Jamhuri ya Czech ambapo walikuwa wageni na walipandishwa Mlima Kilimanjaro na kampuni ya utalii ya Mikaya Tours.

"Ndege ya kampuni ya Kilimedair inayofanya kazi za uokoaji Mlima Kilimanjaro imepata ajali maeneo ya bonde la barafu majira ya saa 11:30 jioni, helikopta ilikuwa na watu watano na watu wote wamefariki dunia," amesema Kamanda Maigwa.

Taarifa kutoka eneo la tukio ambazo bado hazijathibitishwa zinaeleza kuwa baada ya helikopta hiyo kuanguka ililipuka moto na kusambaratika huku jitihada za uokoaji zikifanyika.

Eneo la Kibo Hut na Barafu Camp ni urefu wa kati ya mita 4,670 na mita 4,700 kutoka usawa wa bahari.

Tags: AjaliHelikoptaKilimanjaroMlimaWaathirikawametambuliwa
TNC

TNC

Next Post

Viongozi wa dini: Krismasi iwe daraja la msamaha, umoja wa kitaifa

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company