Saturday, March 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Serikali yatoa siku 90 wasiosajili maeneo ya kazi

by TNC
December 23, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Serikali yatoa Mwongozo wa Miezi Mitatu kwa Wamiliki wa Maeneo ya Kazi Kujisajili OSHA

Dar es Salaam – Serikali imetoa siku 90 (miezi mitatu) kuanzia Januari Mosi kwa wamiliki wa maeneo ya kazi nchini ambao maeneo yao hayajasajiliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kusajili maeneo hayo, kinyume na hapo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Agizo hilo la Serikali limetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za OSHA zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na menejimenti na watumishi wa wakala huo, Jumatatu Desemba 22, 2025, Sangu amesema taasisi hiyo ina dhamana ya kulinda nguvu kazi ya Taifa dhidi ya ajali, magonjwa na vifo vitokanavyo na mazingira ya kazi yasiyokuwa rafiki.

Aidha, amesema ili OSHA isimamie ipasavyo uzingatiaji wa kanuni bora za usalama na afya katika maeneo ya kazi nchini, yanapaswa kutambulika na kupata usajili.

Waziri huyo amewataka watumishi wa OSHA kufanya kazi kwa bidii, kujituma na kuzingatia weledi katika kuwawezesha waajiri kusimika mifumo madhubuti ya usalama na afya mahali pa kazi.

"Usajili wa sehemu za kazi nchini ni kwa mujibu wa kifungu cha 16 na 17 cha Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003 ambapo OSHA husajili maeneo ya kazi na kisha kuyafikia kwa ajili ya ukaguzi na ushauri wa kitaalam juu ya uboreshaji wa mazingira ya kazi," ameeleza Waziri Sangu.

Awali akizungumza, Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda amesema wamepokea maelekezo ya Waziri na wako tayari kwa utekelezaji.

"Kwa niaba ya watumishi wenzangu, nikuhakikishie kwamba hatutakubali kuwa sababu ya kukwamisha utendaji wenu bali tutajitahidi kutekeleza majukumu yetu ipasavyo, na hivyo kuwafanya nyinyi viongozi wetu kutembea kifua mbele kutokana na utendaji wetu mzuri," amesema.

Tags: kaziMaeneoSerikaliSikuwasiosajiliyatoa
TNC

TNC

Next Post

Hujachelewa kumtafutia mtoto shule bora

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company