Sunday, December 14, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Chalamila aitaka taasisi ya maji kuja na suluhu ya kudumu uhaba wa maji jijini

by TNC
December 13, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Tatizo la Upungufu wa Maji Dar es Salaam Laweza Kusababisha Mgogoro wa Kisiasa

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ameonya kuwa upungufu wa maji unaweza kusababisha mgogoro mkubwa kati ya wananchi na Serikali, hali inayoweza kuhatarisha utulivu wa kisiasa na usimamizi wa jiji hilo.

Chalamila ametoa kauli hiyo Jumamosi, Desemba 13, 2025, wakati wa ziara yake ya kukagua uzalishaji wa maji katika Mto Ruvu na visima vya kuyahifadhi na kuyasambaza katika eneo la Kimara jijini humo.

"Maji yakikosekana tutazalisha mgogoro mkubwa sana kati ya wananchi na Serikali. Mtu mwenye kiu atawezaje kutii sheria? Kutakuwa na mtikisiko wa kisiasa na jiji halitatawalika," amesema.

Wito wa Mkutano wa Dharura

Kutokana na hali hiyo, amewataka wajumbe wa bodi za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) na Bodi ya Bonde la Wami–Ruvu kukaa pamoja na kutafuta suluhisho la kudumu la uhaba wa maji unaolikabili jiji hilo.

Katika vyanzo hivyo, Chalamila ameshuhudia jinsi maji yalivyopungua kwa kiwango kikubwa baada ya maeneo unakopita Mto Ruvu kukosa mvua muda mrefu.

Ameonya kuwa iwapo hali itaendelea kwa wiki mbili zaidi bila hatua madhubuti, athari zake zitakuwa kubwa kwa wananchi, viwanda na pato la Taifa.

Bwawa la Kidunda Tegemeo la Baadaye

Chalamila amesema maji yatakayopatikana kutoka Mradi wa Bwawa la Kidunda, ingawa nalo linategemea mvua, yakihifadhiwa na kusimamiwa ipasavyo, yataweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuhudumia wakazi wa Dar es Salaam na kupunguza changamoto ya upungufu wa maji.

Bwawa la Kidunda lililopo mkoani Morogoro, lilianza kujengwa na Serikali mwaka jana na sasa ujenzi wake umefikia asilimia 35, likitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2026.

Mto Ruvu Una Tabia ya Ukame

Mkuu wa mkoa amesema kulingana na maelezo yaliyopewa na wataalamu, Mto Ruvu una tabia ya ukame unaojirudia takribani kila baada ya miaka mitano, hivyo Dawasa kwa kushirikiana na Bodi ya Bonde la Wami–Ruvu, wanapaswa kutafuta suluhisho la kudumu la kukabiliana na hali hiyo.

Ameshauri mipango ya muda mrefu izingatie mabadiliko ya tabianchi na kasi ya ukuaji wa Jiji la Dar es Salaam, ambalo linakadiriwa kufikia wakazi zaidi ya milioni 10 mwaka 2030.

"Dar es Salaam ni miongoni mwa majiji saba yanayokua kwa kasi barani Afrika. Ifikapo 2030 litakuwa na zaidi ya watu milioni 10. Ikifika wakati huo, vyanzo vya sasa vya maji vitatosha? Lazima tuangalie mbele," amesema.

Mpango wa Bwawa la Nyerere

Ameongeza kuwa hata mradi wa Bwawa la Kidunda unategemea mvua ambazo hazitabiriki, hivyo ni muhimu kujiandaa kwa hali ambayo itasaidia ikiwa mvua hazitanyesha labda kwa miaka miwili mfululizo.

Chalamila pia ameunga mkono pendekezo la kutumia maji kutoka Bwawa la Nyerere lililopo Mto Rufiji, akibainisha kuwa mradi huo upo katika hatua za maandalizi ya zabuni.

Vilevile, ameshauri mamlaka za maji kuangalia uwezekano wa kushirikisha sekta binafsi katika hatua za uzalishaji, usafirishaji au usambazaji wa maji, ili kupunguza tatizo linaloongezeka kutokana na ongezeko la idadi ya watu.

Hali Mbaya ya Uzalishaji wa Maji

Mkurugenzi wa Bodi ya Bonde la Wami–Ruvu, Elibariki Mmasi, amesema hali ya uzalishaji wa maji ni mbaya kutokana na uhaba wa mvua uliodumu kwa miezi saba hadi minane katika maeneo ya Mto Ruvu.

Amesema ili kukabiliana na hali hiyo, bodi imesitisha vibali 250 vya matumizi ya maji kwa shughuli zisizo za majumbani, ili maji machache yaliyosalia yaweze kuwafikia wananchi, japo kwa mgawo.

Vilevile, amesema wanafanya doroa ya mara kwa mara kuhakikisha chanzoi hicho kinalindwa huku wakiandaa maneo mahususi ya wafugaji kunywesha mifugo yao.

Tags: AitakaChalamilajijinikudumukujamajisuluhuTaasisiUhaba
TNC

TNC

Next Post

Siri ya Jenista Mhagama kuitwa kiraka

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company