Tuesday, March 17, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Miradi yote ya umwagiliaji itakamilika, Tume mjipange

by TNC
December 12, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Mtwara – Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo ametangaza kwamba Serikali itahakikisha miradi yote ya umwagiliaji inakamilika na kuleta tija kwa wakulima, hatua ambayo itaimarisha uchumi na kuleta uhakika wa chakula nchini.

Chongolo alisema hayo Ijumaa, Desemba 12, 2025 wakati wa ziara yake katika mradi wa umwagiliaji uliopo wilayani Masasi, mkoani Mtwara unaoendeshwa eneo la Ndanda na Tume ya Umwagiliaji.

Mradi huo unahusisha ujenzi wa bwawa la umwagiliaji na uchimbaji wa mifereji mirefu na ukikamilika unatarajiwa kunufaisha zaidi ya wakulima 700 kutoka vijiji saba.

"Serikali itahakikisha miradi yote ya umwagiliaji inakamilika na kuleta tija kwa wakulima hali itakayoimarisha uchumi na kuleta uhakika wa chakula," amesema Chongolo.

Waziri amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa bwawa hilo ambalo litachochea matumaini mapya kwa wakulima wa Mtwara kwa kuwawezesha kulima mazao mbalimbali ikiwemo mbogamboga, mpunga, mahindi na mazao mengineyo.

Chongolo amesema ingawa Mtwara inasifika kwa kilimo cha korosho, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) imeanzisha miradi ya umwagiliaji katika mikoa ya Lindi na Mtwara ili kuhamasisha uzalishaji wa mazao mengine ndani ya mikoa hiyo bila kutegemea mazao kutoka maeneo mengine.

Waziri huyo ameitaka tume hiyo kusimamia kwa umakini miradi hiyo ili kuhakikisha thamani ya fedha iliyowekezwa inaonekana na wakulima wanapata uzalishaji unaoendana na viwango vinavyotakiwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Raymond Mndolwa amesema Serikali imewekeza na inaendelea kuwekeza fedha nyingi kuhakikisha wananchi wa Lindi na Mtwara wananufaika na miradi ya umwagiliaji, hatua ambayo itawawezesha kufanya kilimo cha uhakika bila kutegemea mvua.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainabu Telacky amewataka wananchi kushirikiana na Tume katika kulinda miundombinu na rasilimali zilizowekezwa na Serikali kwa kuwa wao ndio wanufaika wakuu wa mradi huo.

Akitoa taarifa ya mradi huo, Mhandisi Macklera Mrutu kutoka Tume amesema kuna jumla ya miradi 26 ya umwagiliaji katika mikoa ya Lindi na Mtwara yenye thamani ya Sh23.7 bilioni. Hadi sasa miradi miwili imeanza utekelezaji ikiwemo ujenzi wa mabwawa na mifereji mirefu, ambayo itachukua hekta zaidi ya 300 na utekelezaji wake umefikia asilimia 27.

Tags: itakamilikamiradimjipangeTumeUmwagiliajiYote
TNC

TNC

Next Post

Deputy minister suspends six Kilolo council officials over alleged misuse of funds in girls' school project

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company