Thursday, March 19, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Waziri wa zamani Mwambe amekamtwa na polisi

by TNC
December 12, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Polisi Yathibitisha Kumshikilia Waziri wa Zamani Geofrey Mwambe

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limethibitisha kumshikilia Waziri wa zamani, Geofrey Mwambe, tangu usiku wa Desemba 7, 2025 alipokamatwa katika eneo la Tegeta, Kinondoni, kwa tuhuma zinazohusiana na makosa ya jinai ambayo bado hayajatajwa, yanayoendelea kuchunguzwa.

Taarifa ya polisi iliyotolewa leo Desemba 12, 2025 imeeleza kuwa Mwambe, waziri wa zamani wa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na baadaye Viwanda na Biashara, alikamatwa wakati wa operesheni ya kawaida ya ufuatiliaji wa matukio ya usalama jijini Dar es Salaam, na kwamba hatua za awali za kisheria kuhusu tuhuma hizo zinaendelea kukamilishwa.

Mwambe aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), mbunge wa Masasi, Mtwara (CCM), ameshikiliwa na Jeshi la Polisi tangu Desemba 7, 2025 na baada ya kimya kutawala juu yake, jana Desemba 11, 2025 Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP), Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam (ZCO), walifunguliwa mashtaka mahakamani kwa kumshikilia kinyume na sheria.

Shauri hilo la maombi namba 289778/2025 lilifunguliwa na Mwambe akiwa mwombaji kupitia kwa wakili wake, Hekima Mwasipu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya hati ya dharura na lilipangwa kusikilishwa Desemba 15, 2025.

Mbali na taarifa hiyo, Polisi imetoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu na kuviachia vyombo vya dola kukamilisha taratibu za uchunguzi na hatua za kisheria.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, kulitaka Jeshi la Polisi kuzingatia ukamataji wa staha na kufuata sheria za nchi.

Tags: amekamtwaMwambePolisiWaziriZamani
TNC

TNC

Next Post

Government launches nationwide public service audit

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company