Sunday, December 7, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Watano wakamatwa kwa udanganyifu wa tiketi

by TNC
December 6, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Watu Watano Wakamatwa Kwa Ulanguzi wa Tiketi Kituo cha Magufuli

Dar es Salaam – Watu watano wamekamatwa wakituhumiwa kulangua tiketi katika ukaguzi uliofanyika na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra) kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli.

Watuhumiwa hao walikamatwa Desemba 5 na 6, 2025.

Baadhi ya watuhumiwa wanadaiwa kukutwa na tiketi 20 hadi 30 kutoka kampuni tofauti za mabasi, wakiziuza kwa bei kubwa kuliko bei elekezi, kisha kuwapeleka abiria kwenye mabasi wasiyoyafahamu.

TNC ilipokea taarifa kuhusu ulanguzi wa tiketi katika kituo hicho kutokana na kile kinachoonekana mabasi kujaa hadi Desemba 8, kwa mujibu wa mfumo wa ukataji tiketi mtandaoni.

Hata hivyo, kinachoonekana ni kuwa kuna baadhi ya watu waliokata tiketi na kizihodhi kisha kuziuza kwa wasafiri waliozikosa kwa gharama waitakayo, licha ya kuwa zimeandikwa kiwango halali cha nauli.

Latra Yawasihi Abiria Kununua Tiketi za Kielektroniki

Akizungumza Desemba 6, 2025 Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Latra, Habibu Suluo amesema kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wamewakamata mawakala wasio rasmi ambao hawajasajiliwa, maarufu masarange, wanaowadanganya abiria kwa kuuza tiketi za karatasi zisizo halali.

"Kuna wengine wamekuwa wakiwatumia abiria kwa kuwauzia tiketi za bei juu, na ukifika kwenye basi unakuta nauli halisi ni ndogo au basi lenyewe halipo kabisa," amesema.

Suluo amesema baadhi ya kampuni zimehusika, zikiwamo zinazofanya safari ya Lushoto ambao wamepandisha nauli kwenye tiketi za karatasi, ingawa tiketi za mtandao zilionyesha bei halisi.

Amesema abiria wote waliotozwa zaidi wameelekezwa kurejeshwa fedha zao, huku kampuni na wahusika wakitozwa faini.

Suluo amesema watu waliokamatwa wako chini ya ulinzi na taratibu za kuwafikisha katika vyombo vya sheria zinaendelea.

"Tunataka iwe fundisho kwa nini udhulumu watu wakati biashara ni huru? Fanya kazi, lipwa haki yako, lakini siyo kuumiza abiria," amesema.

Latra imewasihi abiria kuhakikisha wanalipia tiketi za kielektroniki na kuepuka kununua za karatasi zinazoandikwa kwa mkono na watu mitaani.

Vibali vya Dharura Vimetolewa

Wakati huohuo, Suluo amesema mamlaka imetoa vibali vya dharura 72 vya mabasi ili kukabiliana na ongezeko la abiria lililotokea mwanzoni mwa Desemba kutokana na shule kufungwa na ratiba za watu wengi kusafiri. Amesema kwenye kituo cha Magufuli vimetolewa vibali 31.

Suluo amesema hali ya usafiri kwa sasa imetulia tofauti na siku tatu zilizopita ambapo msongamano ulikuwa mkubwa.

Wakala Anakiri Kuongeza Nauli

Wakala Salma Maganga, amekiri wamekuwa wakiongeza nauli kipindi cha msongamano wa abiria, akisema kitendo hicho kimetokana na ukosefu wa mafunzo, presha ya abiria wengi na magari machache.

Amesema siku ya tukio abiria walikuwa wengi kuliko kawaida, hali iliyowafanya mawakala wengine kutafuta pesa ya maji, ili kumpa abiria uhakika wa kupata siti, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

"Kosa nililofanya ni kuongeza nauli tofauti na halisi ambayo ni kutoka Dar es Salaam hadi Handeni ni Sh17,000, lakini tulimwambia abiria atuongezee hela ya maji ili apate siti kama tunavyojua hali ni ngumu," amesema na kuongeza:

"Walipokuja Latra kutukagua, tukakubaliana turudishe fedha tulizowazidishia abiria. Tumerudisha zote," amesema.

Pia, amekiri kutokuwa na mafunzo kamili kutoka Latra na kwamba bado hajasajiliwa kuwa wakala anayeruhusiwa kufanya biashara hiyo.

Abiria Walalamika Nauli Tofauti

Sophia Kanegene, abiria aliyekuwa kituoni hapo amesema alitishiwa kushushwa kwenye basi baada ya kuona ametozwa nauli tofauti na wengine na nauli elekezi.

Amesema safari yake ni ya Geita – Katoro, ambapo awali alielezwa nauli ni Sh35,000 hadi Geita, kisha angeongeza kiasi kingine kutoka Geita kwenda Katoro. Hata hivyo, alipofika stendi, alilazimishwa kulipa zaidi.

Sophia anasema baada ya kupata tiketi, alitambua kuwa nauli aliyotozwa abiria ni tofauti hata kama safari ilikuwa moja. Tiketi zilikuwa zimeandikwa jina la Pendo na bei haikufanana.

"Tiketi zetu zinafanana, zimeandikwa Pendo cha ajabu nimetozwa Sh35,000, mwingine Sh40,000, mwingine Sh75,000. Yule aliyekuwa anaenda Kigali ametoa Sh75,500. Mwingine aliyekuwa anaenda Geita ametozwa Sh57,500 safari ni moja, lakini bei zinatofautiana," amesema.

Amesema askari polisi walifika stendi na kuanza kuhoji wahusika, jambo lililowapa abiria nafasi ya kueleza yaliyotokea.

Tags: kwaTiketiUdanganyifuWakamatwaWatano
TNC

TNC

Next Post

Underperforming public entities face possible merger or dissolution

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company