Sunday, December 7, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Mfaransa kuwekeza ujenzi Bandari ya Bagamoyo

by TNC
December 6, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Dar es Salaam. Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesaini hati ya Makubaliano na Kampuni ya Africa Global Logistics (AGL) kwa ajili ya usanifu, ujenzi na uendeshaji wa gati mpya tatu katika Bandari ya Bagamoyo.

Hati ya makubaliano (MoU) imesainiwa Desemba 6, 2025 Makao Makuu ya TPA jijini Dar es Salaam kati ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa na Rais wa AGL, Philippe Labonne.

Mbossa amesema kusainiwa kwa hati ya makubaliano hayo ni ishara ya utayari wa kuanza kwa mradi wa bandari mpya ya Bagamoyo ambapo kwa kuanzia AGL itaanza usanifu na ujenzi wa gati tatu mpya za kisasa kati ya 28 zinazotarajiwa kujengwa katika bandari hiyo pamoja na gati mbili mpya za kisasa katika Bandari ya Dar es Salaam.

"Tunategemea kuanza ujenzi wa gati mpya tatu katika Bandari ya Bagamoyo mapema mwezi Januari na pia tunawakaribisha wawekezaji wengine wa ndani na wa nje katika mradi huo ambapo lengo ni kuleta mapinduzi makubwa katika shughuli za kibandari nchini," amesema Mbossa.

Kwa upande wake Rais wa AGL, Philippe Labonne, amesema wameamua kuingia makubaliano na TPA na kuwekeza Tanzania kutokana na kuwa nchi yenye amani, usalama na mazingira bora ya uwekezaji iliyosehemu sahihi kijiografia kwa sekta ya uchukuzi na kuwa lango la biashara kitaifa na kimataifa.

"Ninaamini Tanzania ni nchi inayokuwa kwa kasi kimaendeleo ikiwa na mtaji mkubwa wa watu wakarimu na mtazamo chanya. Pia ni lango la kuingilia nchi nyingi barani Afrika na kuyafikia masoko ya kimataifa, hivyo naamini ushirikiano huu utafungua mambo mengi ikiwemo kutengeneza ajira ambazo ni muhimu kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla," amesema Labonne.

Mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kwa gati mpya tatu utajengwa kwa miezi 36 (miaka mitatu).

Kampuni ya AGL imepata nafasi hii ya kushirikiana na TPA katika ujenzi huo kutokana na uzoefu wao kama kampuni kubwa ya huduma za usafirishaji na logistiki.

Kampuni hii inatoa huduma kamili za usafirishaji, usimamizi wa mizigo, usafirishaji wa kimataifa na huduma za forodha, ikihudumia sekta mbalimbali kama uchimbaji, mafuta, chakula, na misaada ya kibinadamu.

Tags: BagamoyoBandarikuwekezaMfaransaujenzi
TNC

TNC

Next Post

Wildfire sweeps across Mount Hanang in Tanzania as authorities rule out volcanic activity

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company