Sunday, December 7, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Mwigulu asema kuna mchezo unachezwa

by TNC
December 5, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Waziri Mkuu Awaonya Vijana Wanaochochewa Kufanya Fujo

Mwanza – Waziri Mkuu wa Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba amewaonya vijana wanaochochewa kufanya vuruga kufumbua macho akisema kuna mchezo unaochezwa.

Dk Mwigulu ametoa onyo hilo Ijumaa Desemba 5, 2025 alipozungumza na wakazi wa Kisesa mkoani Mwanza mara baada ya kukagua ofisi ya Mtendaji wa Kata hiyo iliyochomwa moto Oktoba 29, 2025.

Dk Mwigulu amesema kama kuna mambo yanahitajika kurekebishwa nchini yatarekebishwa kwakuwa Tanzania ni mwalimu wa ukombozi.

"Kama kuna mambo tunahitaji kurekebishwa, Tanzania ni mwalimu wa Ukombozi. Twendeni tuambizane tusije kurudisha nchi yetu kwenye tukio la aina hiyo tena … hatuwezi tukaruhusu uhalifu utawale," amesema Dk Mwigulu.

Ameongeza, "Wale wanaochochewa fungueni macho … wanaowachochea wanalipwa."

Amesema kama ni kilio cha ajira Serikali imeendelea kutekeleza shughuli mbalimbali zinazotengeneza ajira ikiwemo programu za umwagiliaji na viwanda.

"Lakini si watu kuwapa fedha vijana kuhamasisha fujo … amkeni wana mchezo ambao wanacheza na anayecheza yupo kule … Amkeni," amesema.

Uharibifu wa Mali ya Umma

Akizungumzia uharibifu wa miundombinu iliyoharibiwa likiwemo jengo la Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kisesa, Dk Mwigulu amesema majengo yaliyoharibiwa si mali ya Serikali bali ya Umma kwakuwa yametokana na fedha za wananchi.

"Hakuna mkulima anayelima halafu akaenda kuwasha moto shamba lake mwenyewe … hakuna sababu yoyote ile inayokuhamasisha kuchoma nchi yako," amesema.

Amewataka wananchi kwenda kwenye ofisi za umma kuwasilisha kero, changamoto au malalamiko ili yafanyiwe kazi huku akiwaonya watendaji kuwa Serikali haitokuwa na mzaha kwa wasiokuwa na maadili.

Amewahakikishia wananchi kuwa, yale yaliyoahidiwa kwenye kampeni na Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Ilani ya CCM yataanza kutekelezwa ndani ya siku 100 za uongozi wa awamu hii, kwa kuanzia na suala la bima ya afya, kuzuiliwa kwa maiti mahospitalini pamoja na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Taarifa ya Mkoa

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda amemwambia Dk Mwigulu kuwa vuruga mkoani Mwanza zilianzia kwani vijana walianzia eneo hilo kuharibu mali na baadaye kusambaa katika maeneo mengine.

Mtanda amesema uharibifu uliofanyika katika kata ya Kisesa umewakosesha wananchi huduma za kikodi, mabaraza ya ardhi, mikopo ya vikundi na huduma za kimahakama.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Magu, Mohamed Ntandu amesema Oktoba 29, 2025 uchaguzi ulienda vizuri hadi muda wa kufunga vituo, fujo zilianza wakati wa uhesabuji wa kura.

Amesema majengo yaliyoharibiwa ni jengo la ofisi ya Kata ya Kisesa, Mahakama, ofisi ya Tarafa ya Sanjo, jengo la Kata ya Bujora, ofisi ya watendaji wa vijiji na shule za msingi mbili ikiwemo ya Bujora.

Amesema ofisi hizo zinatoa huduma kwa wananchi zaidi ya 65,335, huduma hizo ni pamoja na huduma za kikodi, huduma za ardhi, za vikundi, za ugani, mabaraza ya ardhi ya kata pamoja na huduma za kimahakama.

Dk Mwigulu pia amekagua uharibifu wa miundombinu ya kiwanda cha magodoro ya Banco, ofisi za Maboto Microfinance, ofisi ya Mtendaji Kata ya Nyasaka wilayani Ilemela.

Akiwa Kata ya Nyasaka Wilaya ya Ilemela, Mtanda amesema kutokana na kuharibiwa kwa moto ofisi ya mtendaji wa kata hiyo, zaidi ya wananchi 41,000 wamekosa huduma mbalimbali huku hasara iliyopatikana ni zaidi ya Sh35 milioni.

Tags: asemaKunamchezoMwiguluunachezwa
TNC

TNC

Next Post

Start-up Association unveils ambitious vision to transform the innovation ecosystem

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company