Sunday, December 7, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Mahakama kuamua leo usikilizwaji shauri la kufutwa sherehe za Uhuru

by TNC
December 2, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Mahakama Kuu Kutoa Hatima ya Shauri la Kufutwa kwa Sherehe za Uhuru

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Masjala Kuu Dodoma, leo Jumanne, Desemba 2, 2025 inatoa hatima ya usikilizwaji wa shauri la uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuta sherehe za maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika za Desemba 9, 2025.

Shauri hilo limefunguliwa na Wakili Peter Madeleka, dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kufuatia uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kufuta sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanganyika za Desemba 9, 2025.

Tanganyika ilipata uhuru Desemba 9, 1961 na tangu wakati huo imekuwa ikifanya sherehe kuadhimisha siku ya Uhuru.

Hata hivyo, mwaka huu 2025 sherehe za maadhimisho hayo hazitafanyika.

Novemba 24, 2025, Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba aliutangazia umma kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amefuta sherehe hizo, na fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya maadhimisho hayo zitatumika kukarabati miundombinu ya umma iliyoharibiwa wakati wa vurugu za maandamano ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Historia ya Kufutwa kwa Sherehe za Uhuru

Hii ni mara ya tano kwa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanganyika kufutwa.

Awali, mwaka 2015 Rais wa awamu ya tano, hayati John Magufuli alifuta sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru akaelekeza badala ya kukutana pamoja, maadhimisho hayo yatumike kwa ajili ya kufanya shughuli za usafi nchi nzima.

Fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hizo alielekeza zitumike kufanya upanuzi wa Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, kuanzia eneo la Morocco mpaka Mwenge, jijini Dar es Salaam.

Alisema hatua hiyo itapunguza msongamano wa magari katika barabara hiyo inayotumiwa na watu wote badala ya sherehe ambazo zingetumiwa na watu wachache tu.

Mwaka 2018, Rais Magufuli alifuta sherehe hizo na fedha zilizotengwa akaelekeza zitumike kuanzisha ujenzi wa Hospitali ya Uhuru jijini Dodoma, huku mwaka 2020 akifuta sherehe hizo na fedha akaelekeza zitumike kununulia vifaa vya hospitali ya Uhuru.

Mwaka 2024, Rais wa Samia pia alifuta sherehe hizo na akaelekeza fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili hiyo zitumike kwa shughuli za huduma za kijamii.

Shauri Mahakamani

Hata hivyo mara hii uamuzi wa Rais Samia kufuta sherehe za maadhimisho ya siku hiyo ya Uhuru 2025, umefikishwa mahakamani.

Wakili Madeleka amefungua shauri la maombi ya ruhusa ya mahakama kufungua shauri la mapitio ya Mahakama kupinga uamuzi huo wa Rais.

Shauri hilo lililofunguliwa mahakamani hapo Novemba 26, 2025 lilipangwa kusikilizwa upande mmoja na Jaji Juliana Masabo, Novemba 28, 2025.

Hata hivyo, siku hivyo upande wa wajibu maombi kupitia Wakili kutoka Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali baada ya kupata taarifa hizo ulifika mahakamani na kueleza kuwa hawajapata nakala za shauri hilo.

Hivyo ulipinga shauri hilo kusikilizwa siku hiyo upande mmoja ukaomba liahirishwe mpaka wao watakapopewa nakala za nyaraka hizo.

Hatua hiyo pia ilipingwa na Wakili Madeleka pamoja na mambo mengine alidai kuwa kikanuni shauri hilo, katika hati ya maombi ya kibali linasikilizwa upande mmoja.

Hivyo alidai kuwa kuwapatia au kutowapatia nyaraka hizo hakuwezi kuzuia usikilizwaji wake kwa kuwa hata kama wangekuwa nazo hawawezi kusema lolote.

Kutokana na mabishano hayo, Jaji Masabo baada ya kusikiliza hoja za pande zote aliahirisha shauri hilo mpaka leo Desemba 2, 2025 kwa ajili ya uamuzi wa ama kuendelea na usikilizwaji au kuahirishwa mpaka wajibu maombi watakapopewa nyaraka hizo.

Maombi ya Wakili Madeleka

Katika hati ya maombi ya shauri hilo aliyoiwasilisha mahakamani, Wakili Madeleka anaomba ruhusa ya mahakama hiyo kufungua shauri la kupinga uamuzi huo kwa utaratibu wa mapitio ya mahakama, kuomba amri tatu, zikiwamo ya mahakama ya kufuta uamuzi huo wa Rais wa kufuta sherehe hizo, anaouita kuwa si halali na usio na maana, amri ya kumlazimisha kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sheria na amri ya zuio dhidi yake.

Katika kiapo chake na hati ya maelezo yake zinazounga mkono maombi hayo, Wakili Madeleka anadai kuwa uamuzi huo wa Rais kufuta sherehe hizo alioutoa kupitia kwa Waziri Mkuu Novemba 24, 2025, uliripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari.

"Sherehe hizo zilizoelezwa kwenye hapo juu huadhimishwa kihalali kila mwaka Desemba 9 na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kuenzi Uhuru wa Tanganyika wa Desemba 9, 1961 chini ya uratibu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," anasema.

Madeleka anasema kuwa yeye ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mkazi wa Dar es Salaam, ambaye ana haki ya kusherehekea sherehe hizo, chini ya uratibu wa Serikali kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo, anadai kuwa endapo sherehe za maadhimisho ya siku hiyo za mwaka 2025 hazitafanyika, haki zake zitaguswa kwa kadiri sherehe hizo zinavyomuhusu, kwani yeye ni mnufaika halali wa sherehe hizo.

Kwa msingi huo Madeleka anasema kuwa ndio maana anaomba ruhusa ya kufungua shauri la mapitio ya mahakama kupinga uamuzi huo wa Rais kufuta sherehe hizo ili aombe mahakama itoe amri hizo tatu.

Msingi wa Kisheria

Wakili Madeleka anadai kuwa anakusudia kuomba amri hizo, kutengua uamuzi wa Rais ili kuheshimu sheria zilizowekwa za kuadhimisha Uhuru wa Tanganyika wa Desemba 9 1961.

Anaeleza Sheria ya Siku za Mapumziko ya Umma Sura ya 35 Toleo la 2023 inaelekeza kuwa Uhuru wa Tanganyika uliopatikana tarehe Desemba 9, 1961 utaadhimishwa kila mwaka Desemba 9.

"Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaweka wajibu kwa kila raia wa Tanzania kuzingatia katiba na sheria nyingine za nchi," anaongeza Wakili Madeleka.

Hivyo anaeleza kuwa ataomba amri ya mahakama kumlazimisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutekeleza sheria zilizoanzishwa za kuadhimisha Uhuru wa Tanganyika Desemba 9.

Pia anaeleza ataomba amri ya kumzuia Rais, kuendelea kutekeleza tangazo lake la kusitisha sherehe za kuadhimisha Uhuru wa Tanganyika za Desemba 9, 2025, kwani kusitishwa kwa sherehe hizo hakujafuata utaratibu ni kinyume na Katiba na sheria nyingine za nchi.

"Mjibu maombi wa kwanza (Rais) hawezi kuruhusiwa kutumia mamlaka ambayo hana kisheria au ambayo yanakiuka sheria za nchi", anasisitiza Wakili Madeleka.

Tags: kuamuakufutwaleomahakamashauriShereheUhuruusikilizwaji
TNC

TNC

Next Post

Mwinyi: Zanzibar open for new investment partnerships

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company