Sunday, December 7, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Mgombea pekee wa chama kikuu apigiwa kura nyingi za hapana

by TNC
December 2, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Bariadi. Mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu umemalizika kwa mgombea pekee wa nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Zebedayo King kupigiwa kura nyingi za hapana.

King alikuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo aliyopitishwa na kamati kuu ya CCM, chini ya uenyekiti wa Rais Samia Suluhu Hassan ambapo kura za maoni zimefanyika Jumatatu, Desemba 1, 2025.

Katika kura hizo za maoni, King ambaye ni Diwani wa Sima ameambulia kura nne za ndio dhidi ya 11 za hapana, matokeo yaliyoibua mshangao kwake mwenyewe, na kufanya nafasi hiyo kulazimu mchakato kuanza upya.

Wakati hilo likitokea kwa King, Zawadi Mkilila, Diwani wa Viti Maalumu ameibuka kidedea katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi baada ya kupata kura 15 za ndiyo bila kupingwa hata kwa kura moja.

Wakati Bariadi Mji ikikosa mshindi, upande wa Bariadi Vijijini mambo yalikwenda vizuri baada ya Mayala Shiminji ambaye ni Diwani wa Kasoli kushinda kwa kura 19, dhidi ya mpinzani wake, Isack Masunga wa Kata ya Nkololo aliyeambulia kura tisa.

Wataalam wa masuala ya kisiasa wanasema matokeo ya Bariadi Vijijini yanadhihirisha mwelekeo tofauti katika vipengele vya uongozi, kukubalika kwa Shiminji kutokana na rekodi yake ya kiutendaji na mahusiano na wajumbe.

Akizungumza na TNC, Ibrahimu Kijanga, Katibu wa CCM Wilaya ya Bariadi na Mkurugenzi wa uchaguzi huo, amesema huo ni mchakato wa ndani ya chama.

"Siwezi kusema chochote bali, michakato ndani ya CCM tumemaliza kwa kuzingatia utaratibu wa CCM taifa, hivyo tunapeleka halmashauri ili waendelee na utaratibu. Wanalilia madaraka, ndio maana uchaguzi wa mgombea mmoja umechukua muda mrefu," amesema.

Wanachama wa CCM wilaya ya Bariadi wanasema matokeo hayo yanatoa mwanga mpya kuhusu namna wajumbe wanavyochukua tahadhari na uwajibikaji kabla ya kupitisha majina ya wagombea.

"Kukosa mshindi siyo changamoto, ni ujumbe wa demokrasia. Hii ni CCM mpya," mmoja wa wanachama amesema.

Tags: apigiwaChamahapanaKikuuKuraMgombeanyingipekee
TNC

TNC

Next Post

Mahakama kuamua leo usikilizwaji shauri la kufutwa sherehe za Uhuru

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company