Monday, December 8, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Mchuano kusaka mameya CCM

by TNC
November 30, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

CCM Kuteua Wagombea Umeya wa Majiji na Uenyekiti wa Halmashauri

Dar es Salaam – Kesho macho na masikio yatakuwa kwa wajumbe wa Chama cha Mapinduzi (CCM) nchi nzima, wanaotarajiwa kupiga kura za maoni katika mchuano wa kusaka majina ya mwisho yawatakaowania umeya wa majiji matano na uenyekiti wa manispaa na halmashauri nchini.

Hatua hiyo inakuja baada ya Kamati Kuu ya CCM kukamilisha mchujo kwa wagombea wote walioomba nafasi hizo na kutoa orodha rasmi ya majina yatakayowasilishwa kwa wanachama kupigiwa kura.

Katika mchujo huo, baadhi ya waliokuwa wakitetea nafasi zao wamepitishwa tena, huku wengine wakikosa nafasi hiyo na kuondolewa katika orodha.

Wagombea 1,067 Walichukua Fomu

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi, akizungumza Novemba 30, 2024 Kisiwandui Zanzibar, ametaja majina hayo akisema ni baada ya kufanya mchujo kwa makada 1,067 waliojitokeza kuchukua fomu kuhitaji nafasi hizo.

"Unaweza kuona idadi hiyo ni namba kubwa inayodhihirisha ukubwa wa CCM pamoja na demokrasia. Katika nafasi hizo, wapo waliochukua fomu ya kuwania umeya wa halmashauri ya jiji, jumla yao 76 na waliogombea umeya wa manispaa wako 137," amesema Kihongosi.

Kihongosi amesema wapo waliochukua fomu kuwania uenyekiti wa halmashauri za miji walikuwa 83 na waliochukua fomu kuwania uenyekiti wa halmashauri za wilaya 729, wote Tanzania Bara.

"Upande wa Zanzibar umeya wa halmashauri ya jiji ni mmoja, umeya wa manispaa watu 34 na uenyekiti wa halmashauri za miji walichukua fomu watu saba," amesema.

Jiji la Dar es Salaam: Ushindani Mkali

Katika Jiji la Dar es Salaam, wamepitishwa watatu – Omar Kumbilamoto anayetete nafasi hiyo akichuana na Nurdin Juma (Shetta), Saad Kimji na Robert Banangwa wote ni maarufu na wana nguvu ya ushawishi.

Kumbilamoto anatetea nafasi hiyo kwa mara ya tatu sasa, ya kwanza alikuwa meya wa Ilala kabla ya kupandishwa hadhi kuwa Jiji la Dar es Salaam na atashindana na Shetta ambaye ni msanii na ni kada mzoefu wa chama hicho.

Jiji la Mbeya: Mchuano wa Viongozi

Katika Jiji la Mbeya, yamerejeshwa majina matatu akiwamo aliyekuwa Meya wa Jiji la Mbeya, Dormohamed Issa, kazi itakuwa nzito pale atakapochuana na wapinzani wake wawili kugombea nafasi hiyo.

Issa atachuana na Godwine Mwakyusa ambaye ni diwani wa Itiji, Dormohamed Issa (Isanga) na Benjamin Mwandete wa Uyole watakaopigiwa kura na madiwani kumpata mmoja atakayeongoza jopo hilo.

Dormohamed aliyekuwa meya wa jiji hilo kwa miaka mitano iliyoisha, atakuwa na kazi ya ziada kutetea nafasi hiyo tena dhidi ya wapinzani wake, huku akijivunia uwezo kiuchumi, uzoefu na historia ya kile alichofanya katika uongozi wake.

Jiji la Dodoma: Profesa Mwamfupe Kuchuana na Vijana

Upande wa Jiji la Dodoma, mchuano utakuwa kati ya meya wa zamani Profesa David Mwamfupe, Hamza Makamba (Uhuru) na Almon Chaula wa Makutupora ambao ni madiwani vijana walioingia kwenye baraza kwa mara ya kwanza kwenye uchaguzi huu.

Mmoja kati ya vigogo waliotazamiwa kutoa ushindani mkali lakini wametemwa ni Kamuli Gombo ambaye ni diwani wa Ipagala.

Profesa Mwamfupe na Makamba wanatoka Jimbo la Dodoma lenye kata 21 huku Chaula akitoka Jimbo la Mtumba lenye kata 20.

Majiji Mengine: Mwanza, Arusha na Zanzibar

Jiji la Mwanza yamerudi majina mawili, yumo Sima Costantine Sima na Happynes Steven Ibasa, watakaochuana kumpata mmoja atakayeongoza jiji hilo.

Kwa upande wa Jiji la Arusha, kuna majina ya makada watatu akiwamo Maxmilliam Iranghe, Matuyani Laizer na Credo Kifukwe.

Upande wa Jiji la Zanzibar, mgombea Kamal Abdulsatar Haji ndiye aliyeteuliwa kugombea nafasi hiyo baada ya jina la aliyekuwa meya wa jiji hilo, Mahmoud Mohammed Mussa kutoteuliwa. Hivyo, katika kinyang’anyiro hicho Kamal hatakuwa na mshindani.

Jiji la Tanga walioteuliwa ni Seleboss Mustafa, Joseph Emmanuel, Idd Ally na Hamza Bwanga.

Manispaa: Kinondoni, Ubungo, Temeke na Moshi

Manispaa ya Kinondoni yamerudi majina mawili, Abdulkadir Mgeni atachuana na Songoro Myonge anayetetea kuongoza nafasi hiyo kwa mara ya tatu sasa.

Ingawa ni vigumu kutabiri katika mchuano huo, lakini Songoro Myonge amejijengea umaarufu kwa kupigania changamoto za wananchi wa eneo hilo ingawa jukumu la kumbakiza litaamuliwa na wajumbe.

Ubungo majina matatu yamerudi akiwamo Zaidi Muliro, Ashura Sengondo na Laurence Mlaki, katika majina hayo mbali na wote kuwa maarufu katika siasa za Ubungo, lolote linaweza kutokea kwa kuwa aliyekuwa anatetea hayumo katika mchuano huo.

Manispaa ya Temeke, kamati kuu ya chama hicho imerudisha majina mawili Juma Rajabu Mkenga na Uzairu Athumani katika nafasi hiyo wote hao ni wageni lolote linaweza kutokea kwa kuwa, aliyekuwa meya sasa ni mbunge wa Mbagala.

Manispaa ya Moshi, majina matatu yamepenya likiwamo la Zuberi Kidumo, Stallone Malinda na Deogratias Mallya, kuteuliwa kwao kumechukua mwelekeo mpya wa siasa.

Vita hiyo sasa imebaki kati ya aliyekuwa meya, Kidumo, pamoja na wenzake hao. Awali, kabla ya uteuzi huo, majina yaliyokuwa yakitajwa zaidi katika mchuano wa nafasi hiyo yalikuwa ya Kidumo na Juma Raibu, ambaye aliwahi kuondolewa katika nafasi ya umeya kutokana na tuhuma mbalimbali.

Hata hivyo, baada ya kutotajwa katika uteuzi wa mwisho, wafuasi wa Juma Raibu wamehamishia nguvu zao kwa Malinda, jambo linaloonekana kuibua mwelekeo mpya wa kisiasa ndani ya manispaa hiyo.

Tags: CCMkusakamameyaMchuano
TNC

TNC

Next Post

Graduates shown the key to tackling unemployment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company