Sunday, December 7, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Benki yaanza uhamasishaji wa afya mahali pa kazi

by TNC
November 26, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Dar es Salaam. Kisukari kinaendelea kuwa miongoni mwa changamoto kubwa za kiafya zinazokua kwa kasi nchini Tanzania, huku maelfu ya watu wakiishi na ugonjwa huu bila kujua hali zao.

Uelewa mdogo, kuchelewa kufanya vipimo, pamoja na kuongezeka kwa mitindo ya maisha isiyo rafiki kwa afya ikiwa ni pamoja na ulaji usiofaa, kutofanya mazoezi na msongo wa mawazo vimeendelea kuongeza idadi ya watu wanaoathirika. Matokeo yake ni madhara makubwa kiafya kama matatizo ya figo, kupoteza uwezo wa kuona na hata vifo.

Kwa kutambua ukubwa wa tatizo hilo, Benki ya Exim imechukua hatua kuunga mkono jitihada za utambuzi wa mapema na kuhamasisha maisha yenye afya, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kisukari Duniani 2025.

Benki hiyo imeshirikiana na Chama cha Kisukari Tanzania (TDA) kuendesha shughuli mbalimbali za kitaifa, ikiwa ni ishara ya dhamira yake ya kwenda mbali zaidi ya huduma za kifedha na kuchangia katika ustawi wa jamii.

Katika hatua hiyo, Benki ya Exim imefanya upimaji wa kisukari bure kwa wafanyakazi na wateja wake. Hatua hiyo imeenda sambamba na kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu: "Kisukari na Ustawi Mahali pa Kazi."

Kaulimbiu ya mwaka huu inasisitiza umuhimu wa kutambua dalili mapema, kuimarisha huduma za kinga na kukuza mitindo bora ya maisha ili kupunguza hatari ya kupata kisukari. Kwa kuwaletea wafanyakazi na wateja huduma karibu, benki imewapa nafasi ya kutambua viashiria vya hatari mapema na kujua hatua za kuchukua ili kujikinga au kusimamia ugonjwa huo.

Vipimo vilivyotolewa vilijumuisha tathmini ya mtindo wa maisha, kipimo cha urefu, uzito na BMI, ufuatiliaji wa shinikizo la damu pamoja na kipimo cha sukari kwa kutumia glucometer. Kupitia uchunguzi huo, washiriki walipata fursa ya kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu afya zao na hatua za kuchukua ili kuboresha ustawi wao.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim, Stanley Kafu, alisema afya za wafanyakazi na wateja ni msingi muhimu wa ustawi na tija katika maeneo ya kazi.

"Wafanyakazi na wateja wetu ndio kiini cha kila tunachofanya. Kwa kutoa vipimo hivi, tunalenga kuwapa elimu muhimu ya kujikinga na athari za kisukari," alisema na kuongeza kuwa shughuli hiyo imefanywa kwa kuzingatia viwango vya kitaalamu na usiri wa taarifa za kiafya za washiriki.

Mbali na kampeni hiyo ya kisukari, Benki ya Exim kupitia programu yake ya Exim Cares imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya afya nchini. Miongoni mwa shughuli walizofanya mwaka huu ni uchangiaji damu, kuunga mkono huduma za afya ya akili kwa watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, kutoa vifaa vya matibabu, kufadhili na kutoa elimu kwa ushirikiano na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), pamoja na kutoa elimu ya bure kuhusu saratani ya matiti na saratani kwa ujumla.

Mfululizo wa shughuli hizi unaonesha kwa kiasi kikubwa dhamira ya benki katika kuboresha huduma za afya kwa jamii, pamoja na kujenga maeneo ya kazi yenye ustawi na watu wenye uelewa mpana kuhusu kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.

Benki ya Exim na Chama cha Kisukari Tanzania wanaamini kuwa hatua hizi zitahamasisha mashirika mengine nchini kuwekeza katika afya za wafanyakazi wao. Hii ni kwa kutambua kuwa kupunguza athari za kisukari si jukumu la Serikali pekee bali linahitaji ushirikiano wa karibu kati ya sekta binafsi, taasisi za afya na jamii kwa ujumla.

Kwa ujumla, jitihada za Benki ya Exim zinatoa mfano mzuri wa namna taasisi za kifedha zinavyoweza kuchangia si tu kiuchumi bali pia katika kulinda afya za watu, na hivyo kuijenga Tanzania yenye jamii yenye ufahamu na inayothamini afya mahali pa kazi.

Tags: AfyaBenkikazimahaliuhamasishajiyaanza
TNC

TNC

Next Post

Mwandishi wa televisheni na wengine watatu wafutiwa mashitaka ya uhaini na DPP

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company