Sunday, December 7, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Wanawake waongoza kwa idadi ya wahitimu

by TNC
November 21, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Wahitimu 1,658 Watunukiwa Vyeti na Shahada RUCU, Wanawake Waongoza

Iringa – Chuo Kikuu Katoliki Ruaha (RUCU) leo kimefanya mahafali yake ya 18 katika viwanja vya chuo hicho jijini Iringa, ambapo jumla ya wahitimu 1,658 wametunukiwa vyeti, stashahada, shahada na shahada za uzamili.

Katika mahafali hayo, wanawake wameongoza kwa idadi kubwa, ikiwa ni 920, dhidi ya wanaume 738, hatua inayotafsiriwa kama ishara ya ukuaji wa usawa wa kijinsia katika elimu ya juu nchini.

Mahafali hayo yameenda sambamba na mvua kubwa iliyonyesha alfajiri, jambo ambalo wengi wamelitafsiri kama baraka kwa safari mpya ya wahitimu hao.

Akizungumza katika mahafali hayo, Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Chrispina Lekule amesema ongezeko la wahitimu wanawake linaonyesha mabadiliko chanya katika dhana ya usawa wa fursa za elimu.

"RUCU inaendelea kutoa elimu ya ubunifu na yenye mwelekeo wa kulijenga taifa. Tunaamini wahitimu wetu hususan wanawake watakuwa chachu ya mabadiliko katika jamii zao," amesema Prof. Lekule.

Mgeni rasmi, Askofu wa Jimbo Katoliki la Njombe, Eusebio Kyando amewataka wahitimu kutoridhika na kiwango walichofikia, akisema elimu ni njia isiyokoma.

"Msiridhike na hatua hii. Endeleeni kujiongezea maarifa, kwani taifa linawategemea katika kuliletea mabadiliko," amesema Askofu Kyando.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Linda Selekwa aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa, amekipongeza chuo kwa kusisitiza ubunifu, utafiti na taaluma zenye kuleta suluhisho katika jamii. Amewataka wahitimu kutumia elimu kama "silaha" katika kukabiliana na changamoto za kijamii na kiuchumi.

Sauti za Wanawake Wahitimu

Wahitimu wanawake walionekana wenye furaha na matumaini makubwa kuhusu mustakabali wao, huku kila mmoja akieleza namna atakavyotumia taaluma yake kuleta matokeo chanya kwenye jamii.

Anna Peter aliyehitimu Shahada ya Uuguzi na Ukunga amesema, "Nimetoka kwenye familia ya kipato cha chini, lakini leo ninasimama kama mhitimu. Nitaitumia taaluma yangu kuelimisha akina mama kuhusu afya ya uzazi na kupunguza vifo vya mama na mtoto vijijini."

Joyce Mwakasege aliyehitimu Shahada ya Sheria amesema "RUCU imenipa misingi ya uadilifu na haki. Nitapigania haki za wanawake na watoto kupitia taaluma yangu."

"Nia yangu ni kufungua biashara ndogondogo na kuwahamasisha wanawake kuwa wajasiriamali wenye kujitegemea," amesema Hadija Hassan aliyehitimu Stashahada ya Utawala wa Biashara.

Tags: IdadikwawahitimuWanawakewaongoza
TNC

TNC

Next Post

Ushahidi utakaotumika katika kesi ya Jatu umewekwa wazi

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company