Sunday, December 7, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Bakwata yalaani vurugu ya Oktoba 29 yagusia mariadhiano, suluhu

by TNC
November 14, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Bakwata Yasikitika na Vurugu vya Oktoba 29, Vifo na Uharibifu wa Mali

Dar es Salaam – Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limesikitishwa na vitendo vya vurugu vilivyotokea Oktoba 29, vilivyosababisha watu kupoteza maisha na uharibifu wa mali za umma na binafsi.

Bakwata limesema Oktoba 29, siku ya kupiga kura kulizuka kundi lililokuwa likiwatisha watu, kupora na kuharibu mali, miundombinu mbalimbali ikiwemo kuchoma vitu vya mafuta na ofisi za umma.

Maandamano yaliyozua vurugu hizo yalianzia Dar es Salaam na baadaye katika baadhi ya mikoa kama Arusha, Mwanza, Mara, Mbeya na Songwe zilisababisha taharuki na madhara katika miji mikubwa na kuzua hofu na usumbufu wa shughuli za kila siku na kusababisha kuporomoka kwa mzunguko wa fedha.

Tamko la Bakwata limetolewa Alhamisi Novemba 13, 2024 kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu wa Baraza la Ulamaa la Bakwata, Sheikh Hassan Chizenga limeeleza uhalifu huo uligawanyika katika makundi mbalimbali ikiwemo wapo waliofurahia na waliochukizwa.

"Kutokana na vitendo hivi vya kihalifu, ililazimu vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kudhibiti hali na ndani yake kukatokea vifo vya watu wasiokuwa na hatia."

"Wengine walipata ulemavu wa kudumu, pamoja na uharibifu, wizi na upotevu wa mali, yote haya yakisababishwa na kundi hilo lililokuwa likifanya fujo, wizi na uharibifu mkubwa wa miundombinu," imeeleza Bakwata.

Kutokana na hilo, Bakwata inalaani vitendo vya kihalifu ambavyo udhibiti wake umesababisha vifo vya watu wasiokuwa na hatia.

"Kwa umoja wetu tumesikitika sana kwa haya yaliyotokea hasa maisha ya watu kupotea kutokana na vitendo hivi vya kihalifu. Mafundisho yetu yanasema maisha ya mtu mmoja kupotea ni sawa na kupoteza maisha ya watu wote."

"Ndio maana kwa umoja wetu kabla ya uchaguzi mkuu tumefanya kazi kubwa ya kuhimiza umuhimu wa kutunza amani. Pale haki inapobidi kudaiwa, basi idaiwe kwa utaratibu usiovunja amani na kusababisha maafa makubwa," imeeleza.

Bakwata imesisitiza kulaani vitendo vya kihalifu, likitokea wito kudhibitiwa na kuhakikisha havitokei tena katika Taifa letu.

Sambamba na hilo, Bakwata imeitaka Serikali kufanya uchunguzi kwa kina kuhusu vurugu hizo ili kubaini viongozi wa kuchochea vijana wa Tanzania kufanya uhalifu uliosababisha maisha ya watu kupotea.

"Tunaiomba Serikali kuwaangalia kwa jicho la huruma wale wote ambao kwa namna moja au nyingine wamekumbwa na maafa haya na wala hawakuhusika."

"Katika kipindi hiki tunaisihi Serikali iangalie panapohitajika, kwa maslahi mapana ya nchi yetu. Panapohitaji Suluhu pafanyike kama mafundisho yetu yanavyosema ‘Na Suluhu ni kheri’ surat annisaa aya ya 128."

Pia, Bakwata limefafanua kuwa panapohitaji maridhiano basi Serikali iwe tayari kufanya hivyo kwa maslahi ya mapana ya Tanzania na wananchi wake.

"Ingawa tunaisihi Serikali Suluhu na maridhiano isiwe ni zawadi wanayopewa wale wanaohusika na kushiriki katika uhalifu huu uliosababisha maafa haya," imeeleza.

Tags: BakwatamariadhianoOktobasuluhuvuruguyagusiayalaani
TNC

TNC

Next Post

BoT, NMB risk losing right to defence in microfinance takeover case

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company