Thursday, May 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Lukuvi: Nilijua nitakuwa Spika wa kwanza kukalia kiti hiki, sita kuchuana uspika

by TNC
November 11, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Dodoma. Mbunge mteule wa Isimani (CCM), Mkoa wa Iringa, William Lukuvi amekanusha uvumi ulioenea mitandaoni kuwa aligombea nafasi ya Spika wa Bunge.

Lukuvi ametoa kauli hiyo leo Jumanne Novemba 11, 2025 wakati akitoa maelezo baada ya kuteuliwa kuongoza uchaguzi wa Spika wa Bunge nafasi aliyoipata kutokana na uzoefu wake ndani ya chombo hicho.

Hata hivyo, Lukuvi amesema alitambua angekalia kiti cha Spika kabla ya kuchaguliwa kwa Spika mpya ambaye atakwenda kukalia kiti hicho.

Lukuvi amepewa heshima hiyo ambapo kanuni huwa zinamruhusu Mbunge aliyekaa bungeni kwa muda mrefu mfululizo.

Mbunge huyo aliingia kwa mara ya kwanza bungeni mwaka 1995 ambapo kulikuwa na uchaguzi wa kwanza katika mfumo wa vyama vingi.

"Naomba kufuta uvumi ambao ulienea mitandaoni kuwa nimegombea kiti cha Spika, naomba niseme sikugombea na sikutamani kugombea, ila nilijua ningekalia kiti hiki kama Spika wa kwanza kabla ya Spika atakayechaguliwa," amesema Lukuvi.

Ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wapiga kura wa jimbo lake kwa jinsi walivyomchagua kwa kura nyingi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025.

Uchaguzi wa Spika unaendelea ambapo wagombea wapo sita akiwemo Mussa Zungu wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Wengine ni Veronica Tyeah (NRA), Aniytha Mgaya (NLD), Chrisant Nyakitita (DP), Ndonge Said Ndonge (AAFP) na Amin Yango wa ADC.

Kwa sasa wagombea hao wanajinadi mmojammoja. Baada ya uchaguzi na kumpata Spika kinachofuata itakuwa ni kiapo kwa wabunge wateule.

Tags: HikikitikuchuanakukaliakwanzaLukuviNilijuanitakuwaSitaSpikauspika
TNC

TNC

Next Post

Health risk as pharmacies sell drugs without prescriptions

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company