Sunday, December 7, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Serikali ianzishe maridhiano haraka kuponya majeraha

by TNC
November 6, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Jukwaa la Wahariri Tanzania Lasihi Maridhiano Baada ya Vurugu vya Maandamano

Dar es Salaam. Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeisihi Serikali kuanzisha mchakato wa maridhiano haraka, ili kuponya majeraha kwa pande zote, huku likiwapa pole Watanzania walioguswa na maandamano yaliyozaa vurugu, kadhia mbalimbali na mauaji.

Maandamano hayo yalitokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu Oktoba 29, 2025 katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya, Mwanza, Mara na Arusha.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Novemba 6, 2025 na Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile imeeleza wanafuatilia kwa karibu na wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za vifo vya Watanzania, wakiwamo wanahabari na wengine waliojeruhiwa.

Jukwaa linatoa mwito kwa mamlaka kufanya uchunguzi wa kina na kuhakikisha haki inatendeka.

"Tunaisihi Serikali kuanzisha mchakato wa maridhiano haraka, ili kuponya majeraha kwa pande zote. Tunaomba kila upande mchakato ukianza uwe tayari kushiriki kama nchi tumalize kadhia hii milele," amesisitiza.

Balile amesema, "Jukwaa limerejea utamaduni wa Taifa letu wa amani na utulivu na kuakisi yaliyotokea yakazaa maafa haya. Tunafahamu yapo maumivu makubwa kila upande, ila tunaomba sasa tusimame pamoja kama Taifa, tuzungumze na kujisahihisha, ili kamwe haya yasitokee tena katika ardhi ya Tanzania."

Ripoti za Vifo na Uharibifu

Siku ya tukio jukwaa lilipokea taarifa za vifo vya vijana na askari polisi. Baadhi ya wananchi waliwasiliana na wahariri, kuomba msaada wa kuulizia walipo ndugu zao.

Jukwaa linatoa pole kwa Watanzania waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki katika vurugu zilizotokea katika kilichoanza kama maandamano ya amani, lakini kuishia kwenye uchomaji wa magari, vituo vya mafuta, nyumba, kadhia zingine za kiafya kwa waliopiga kura na hatimaye mauaji ya raia na askari.

"TEF inawakumbuka kwa heshima wanahabari na Watanzania waliouawa katika vurugu hizi, kwani wameacha pengo kubwa katika tasnia ya habari, kazini na familia zao. Pia tunawapa pole wote waliojeruhiwa katika matukio hayo," amesema.

Wito wa Amani na Upatanisho

Taifa limeshuhudia madhara ya amani kupotea na tulikofika, hivyo tujizuie kama nchi isitokee tena.

"Mungu awape uponyaji wa haraka walioumia, azilaze mahali pema peponi roho za waliopoteza uhai, na atupe nguvu ya kusimama kama nchi tujisahihishe. Mungu ibariki Tanzania," amehitimisha.

Tags: harakaianzishekuponyamajerahaMaridhianoSerikali
TNC

TNC

Next Post

Election observers identify electoral gaps, recommend reforms

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company