Sunday, December 7, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Tumia mbinu hizi ukipata kiwewe au mshtuko

by TNC
November 5, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Trauma ya Kisaikolojia: Athari za Matukio ya Kushtua na Jinsi ya Kukabiliana Nayo

Dar es Salaam – Trauma ‘kiwewe’ haitokani na kuumizwa kimwili pekee, bali pia na kile unachoshuhudia.

"Kila nikisikia mlipuko wa tairi, moyo wangu hushtuka," amesema Amina Soud (26), mkazi wa Buguruni mama wa watoto wawili, akieleza jinsi amekuwa akihisi hofu kubwa kila anaposikia mlio wa tairi au fataki.

"Nilikuwa sokoni siku hiyo. Ghafla nilisikia risasi, watu wakapiga kelele. Nilijificha chini ya meza. Tangu siku hiyo, kila sauti kubwa inanifanya nikimbie au nijifiche. Nilijua nimepona, kumbe akili yangu bado iko pale," ameeleza.

Wakati risasi zinapiga, mabomu kulipuka na hofu kutanda, si waliojeruhiwa pekee wanaobeba maumivu – hata waliokuwa mashuhuda hubeba alama za ndani ambazo hazionekani kwa macho.

Mara nyingi, mtu anaweza kuendelea na maisha akidhani amepona, kumbe ndani yake amebeba kiwewe (trauma) kinachoweza kuathiri afya ya akili na mwili kwa muda mrefu.

Dalili za Trauma ya Kisaikolojia

Wataalamu wa afya ya akili wanasema hali kama hii ni ya kawaida kwa watu waliopitia matukio ya kushtua. Wengine hupata usingizi wa shida, ndoto mbaya, au kujiona kama wapo tena katikati ya tukio. Hii huitwa trauma ya baada ya tukio (Post-Traumatic Stress Disorder — PTSD).

Dalili za kukumbwa na hali hiyo kisaikolojia na kihisia ni pamoja na:

  • Kumbukumbu zinazorudia za tukio (flashbacks)
  • Wasiwasi na hasira
  • Hofu na kukosa usingizi
  • Kujitenga na watu au mazingira fulani

Daktari wa Afya ya Akili kutoka Hospitali ya Kanda Mbeya, Dk Raymond Mgeni, amesema janga ni tukio lolote linaloweza kutokea wakati usiotarajiwa na kuleta madhara ya kimwili, kiakili hadi kihesia.

"Matukio kama kusikiliza milio mikubwa ya vitu kama mabomu, kushuhudia tukio la kutisha husababisha msongo mkubwa wa mawazo hata baada ya tukio hilo kujitokeza," ameeleza.

"Hii husababisha wengine kuendelea kulikumbuka tukio, kushindwa kulala, kujawa na woga au wasiwasi au hata kuota ndoto za kutisha. Kisaikolojia matukio haya huweza kusababisha mtu kupata mahangaiko ya kiakili juu ya kukabiliana na tukio lilokwisha kutokea na hivyo huhitaji msaada ili hali isizidi kuwa mbaya zaidi," ameshauri.

Njia za Kupona kutoka Trauma

Dk Mgeni ametaja njia zinazoshauriwa kutumika kwa mtu ambaye amepitia janga:

Kukubali ukweli wa tukio – Hii ni hatua ya awali kabisa ya kuruhusu kupona. Akili ikikataa kuwa hakukuwa na janga huzidi kuteseka zaidi.

Kuepuka mazingira yanayochochea kumbukumbu – Hasa baada ya janga kutokea siku za awali ili kuepusha hali mbaya zaidi ya mahangaiko katika akili.

Kuzungumza au kuandika kile unachopitia – Hili hupunguza maumivu na uchungu unaoweza kuwepo kwa wakati huo.

Kuwa karibu na watu wengine – Wanaoweza kutoa mazingira ya kukutia moyo na matumaini juu ya hatua za kufuata baada ya mshtuko wa janga.

Kutafuta msaada wa kitaalamu – Endapo bado dalili za kushindwa kuvuka dhidi ya janga zikiendelea.

"Epuka matumizi ya vilevi kama pombe, bangi au sigara kama njia ya kusahau maumivu au uchungu. Hili litaongeza madhara mengine mapya kama uraibu wa vilevi kwa siku za baadae," ameshauri Dk Mgeni.

Mshtuko ni Mwitikio wa Kawaida

Daktari bingwa wa magonjwa ya akili Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk Said Kuganda, ameshauri kuwa ni muhimu waliopata trauma ya kisaikolojia wawe na watu wao wa karibu, ndugu wa kuwafariji na wa kuwasaidia, huku wakiepuka kukaa peke yao.

"Kwa kawaida mtu yeyote anaposikia sauti ya risasi au bomu lazima apate mshtuko, ni mwitikio wa kawaida na mara nyingi huendelea kupata mshtuko kwa kipindi cha mwezi mmoja," ameeleza.

Kwa mujibu wa Dk Kuganda, mshtuko utaondoka kwa wengi iwapo mahitaji yao ya kila siku yatarudi ikiwemo vyakula, usafiri, ibada, kazi, shule na mahitaji mengine muhimu.

"Mshtuko ni hali ya kawaida, kuwa na uhakika wa ile amani yako na hofu hupotea taratibu. Mwitikio wa namna ile hatuwezi kusema ni ugonjwa au maradhi, ni mshtuko wa kawaida," amesema.

Ameongeza kuwa kisaikolojia waliopitia majanga kama haya itachukua mwezi mzima kukaa sawa, na kwamba ni muhimu kutoangalia picha mbaya iwe za kweli au za kutengenezwa na akili mnemba.

"Baada ya mwezi kupita wakawa bado hawako sawa, tutasema kuna tatizo watahitaji msaada wa tiba," ameeleza.

Watu Walio Katika Hatari Zaidi

Kwa mujibu wa Dk Kuganda, walio katika hatari ya kupata trauma ni wale waliopoteza wapendwa wao, na kwamba wanahitaji faraja zaidi katika wakati huu. Kundi hilo linaweza kukaa na hali ya huzuni hata miezi sita.

"Wanatakiwa kuwa na watu wa karibu wanaomfariji, huu msiba si wa kawaida. Tongeze kuwafariji ili wawe na matumaini na maombolezo," amesema.

Madhara ya Trauma Isiyoshughulikiwa

Mtaalamu wa saikolojia tiba, Esther Hebron, ameeleza jinsi trauma inavyojidhihirisha kimwili pale isiposhughulikiwa. Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa trauma isipotibiwa huathiri afya ya kimwili.

Tafiti za Adverse Childhood Experiences (ACE) zilionyesha uhusiano mkubwa kati ya matukio ya mshtuko utotoni na matatizo ya kiafya ukubwani. Watu wenye alama za juu za ACE wana uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa sugu kama shinikizo la damu, kisukari na magonjwa ya moyo.

"Trauma isiyoshughulikiwa hujidhihirisha kimwili kupitia maumivu ya kichwa, tumbo, au sehemu nyingine za mwili bila sababu za kiafya zinazojulikana. Pia huleta mabadiliko ya usingizi kama kukosa usingizi, kuamka mara kwa mara usiku au kulala kupita kiasi. Wengine hupata uchovu wa kudumu na kushuka kwa ari ya kufanya shughuli," ameeleza Hebron.

Tafiti za kimataifa zinaonyesha kuwa watu waliopitia trauma wako kwenye hatari kubwa ya kupata wasiwasi, panic attacks, au PTSD, ambazo huambatana na dalili za kimwili kama maumivu ya kichwa na tumbo.

Hebron amesema watu wengi hukimbilia pombe au dawa za kulevya kama njia ya kupunguza maumivu ya kihisia, jambo linaloweza kusababisha utegemezi na matatizo zaidi.

Njia za Kupona

"Ili kupona, ni muhimu kutafuta msaada wa kitaalamu kama ushauri nasaha, CBT au EMDR. Kuongea na watu wa karibu, kushiriki kwenye vikundi vya usaidizi, kufanya mazoezi, kulala vya kutosha, kula vizuri na kujihusisha na shughuli za kiroho au kuandika hisia binafsi husaidia mwili na akili kupona. Kupona kutokana na trauma ni mchakato unaohitaji muda, uvumilivu na kujitunza kwa makini," ameshauri Hebron.

Tags: hizikiweweMbinumshtukoTumiaukipata
TNC

TNC

Next Post

Dk Mwinyi na kiapo bila hotuba

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company