Thursday, October 30, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Mwinyi apiga kura, apongeza wananchi kudumisha amani

by TNC
October 29, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Dk Hussein Mwinyi Apiga Kura Zanzibar

Unguja – Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Hussein Mwinyi, amepiga kura yake katika kituo cha kupigia kura cha Kariakoo viwanja vya michezo ya watoto Jimbo la Kwahani.

Dk Mwinyi alifika katika kituo hicho saa 2:10 asubuhi ya Jumatano, Oktoba 29, 2025 akiwa ameongozana na familia yake, mke wake Mariam na watoto wake watatu.

Baada ya kufika katika kituo hicho, alipanga foleni katika mistari ya wananchi ambao nao walikuwa kwenye foleni kwa ajili ya kupiga kura.

Akizungumza baada ya kupiga kura, Dk Mwinyi amesema ametimiza haki yake ya kikatiba na kwamba amefurahishwa kuona wananchi wamejitokeza kwa wingi kupiga kura.

"Nimetekeleza wajibu wangu kikatiba, nimeshapiga kura, tumeridhika na maandalizi yaliyofanywa na Tume kwakweli ni mazuri," amesema Dk Mwinyi.

Ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi ambao bado wapo nyumbani wajitokeze kupiga kura ili kuwachagua viongozi watakaowatumikia kwa kipindi cha miaka mitano.

Dk Mwinyi amepongeza amani ambayo imetawala kuanzia wakati wa kampeni mpaka asubuhi ya uchaguzi kwani hakuna viashiria vyovyote ambavyo vinetokea kuashiria uvunjifu wa amani.

"Tumefanya kampeni kwa amani kabisa hatukuona chokochoko, mpaka sasa tunaona amani ipo ni imani yetu hali itaendelea hivi hata baada ya kutangazwa matokeo," amesema.

Ametumia fursa hiyo kuwapongeza wapinzani wake 11 anaoshindana nao kujitokeza kuwania nafasi hiyo akisema jambo hilo linaonesha kukuwa kwa demokrasia katika visiwa hivyo.

Hata hivyo, amesema kulingana na kampeni walizofanya wanaamini wananchi wamewakubali na watashinda katika uchaguzi huu.

Mke wake, Mariam amesema: "Siku ya leo tulikuwa tunaisubiria sana tukisema Oktoba 29, imefika kwa hiyo wananchi tujitokeze kwa wingi kupiga kura. Shime shime tujitokeze kwa wingi kupiga kura."

Tags: amaniapigaApongezakudumishaKuraMwinyiWananchi
TNC

TNC

Next Post

Smooth start as residents vote in calm and orderly atmosphere

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company