Thursday, October 30, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Maandalizi ya upigaji kura Kigoma Kusini yakamilika

by TNC
October 26, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Wananchi 259,617 wa Kigoma Kusini Tayari Kupiga Kura Oktoba 29

Uvinza – Wananchi 259,617 wa jimbo la Kigoma Kusini wanatarajia kupiga kura katika uchaguzi mkuu unatarajia kufanyika Oktoba 29, 2025, huku maandalizi yakiwa yamekamilika kwa asilimia mia ikiwa ni pamoja na uwepo wa vifaa vya kupigia kura.

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kigoma Kusini, Acland Kambili, amesema hayo leo Jumapili, Oktoba 26, 2025 wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya wasimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo yaliyofanyika wilayani Uvinza. Kambili amesema idadi ya wananchi hao ndio waliojiandikisha katika daftari la kudumu la mpigakura.

Ameeleza kuwa kuna vituo 660 katika kata 16 za jimbo la Kigoma Kusini na jumla ya wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi 1,980 wanatarajia kupata mafunzo hayo ya siku mbili.

"Nitoe rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura, vifaa vyetu vimewasili na vya kupigia kura na sasa tunavisambaza kwenye vituo husika lakini pia usalama upo wa kutosha kwa kila atakayetoka kwenda kupiga kura siku ya Oktoba 29," amesema Kambili.

Tume ya Uchaguzi Yasisitiza Kufuata Sheria

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jacobs Mwambegele, amewataka wasimamizi wa uchaguzi katika vituo vya kupiga kura kufuata sheria, kanuni na taratibu za INEC kwa muda wote watakaokuwa wanasimamia vituo hivyo, ili kuepusha malalamiko kutoka kwa mawakala wa vyama vya siasa na wananchi kwa ujumla.

"Niwasihi kwa sasa msiache kusoma sheria, miongozo, kanuni na taratibu zilizotolewa na tume lakini pia mkasome Katiba yetu ya Tanzania na kama mtu atakuwa na swali lolote au kuna jambo halijaeleweka tafadhali usiogope kuuliza, lengo ni kujifunza na kutenda haki pamoja na kuwa na uelewa wa kutosha ili ikifika tarehe 29 usibabaike uwe unajua sheria zote na taratibu," amesema Mwambegele.

Amesema wasimamizi hao wajiepushe kuwa chanzo cha malalamiko, wahakikishe vifaa vyote vya kupigia kura viko sawa na vimetimia, kila mmoja afike mapema katika kituo alichopangiwa na ikifika saa 1:00 asubuhi vituo vyote vitatakiwa kuwa wazi na kuanza kupokea wapiga kura.

Wasimamizi Wajitokeza Tayari

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema wapo tayari kwenda kutekeleza majukumu yao kama walivyoapa bila kuegemea upande wa chama chochote.

Benard Jacob amesema siku ya uchaguzi mkuu wataenda kutenda haki kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa kwa hatua zote za upigaji kura hadi kumalizika.

Vumilia Ayoub amesema pamoja na mambo mengine katika mafunzo haya amejifunza kuwapa kipaumbele watu wa makundi maalumu wakiwemo wajawazito, wazee na walemavu, na muhimu katika yote ni kutunza siri ili kuwezesha mchakato mzima wa uchaguzi kuanzia kupiga kura hadi kutangazwa kwa matokeo kumalizika salama.

Tags: KigomaKuraKusiniMaandaliziupigajiyakamilika
TNC

TNC

Next Post

Rais afunga pazia la kampeni, akiahidi neema kwa Wazanzibari

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company