Buzwagi: Ukusanyaji Wa Kimataifa Wa Madini Waanza Shughuli Mpya
Dodoma – Serikali imedokeza kuwa kampuni 15 za kimataifa zimeshapanga kuwekeza katika ukusanyaji maalumu wa madini ulioanzishwa kwenye eneo la zamani la Mgodi wa Buzwagi, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
Mgodi wa Buzwagi, ambao zamani ulikuwa wa pili kwa ukubwa nchini na kuajiri watu zaidi ya 3,000, umefunguliwa rasmi kama Buzwagi Economic Special Zone mnamo Julai 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, alisema eneo hilo sasa lina miundombinu kamili ya maji, majengo, vituo vya uzalishaji wa umeme na barabara.
“Mzunguko wa fedha utarejea moja kwa moja kwa wananchi, ambao watapata nafasi ya kuuza bidhaa zao na kupata ajira mbalimbali,” alisema Mboni.
Pia, mkoa unaendelea na miradi muhimu ikijumuisha mradi wa umeme wa jua wa megawati 150 unaohusisha kijiji cha Ngunga, na ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Ibadakuli – Shinyanga.
Katika awamu ya sita, Mkoa wa Shinyanga umepokea fedha za Sh1.563 trilioni kwa ajili ya maendeleo katika sekta mbalimbali.