Jaji Modibo Sacko wa Jamhuri ya Mali Aitwa Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu
Arusha, Tanzania – Jaji Modibo Sacko wa Jamhuri ya Mali ameteuliwa rasmi kuwa Rais mpya wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR), kufuatia uchaguzi wa siri uliofanyika Juni 2, 2025.
Kabla ya kupata nafasi hii, Jaji Sacko alikuwa Makamu wa Rais wa mahakama hiyo mwaka 2023, akifanya kazi chini ya Jaji aliyekuwa akiongoza awali. Uchaguzi ulihusisha majaji 11 waliopiga kura ya siri katika kikao cha 77 cha kawaida cha Mahakama.
Pamoja na uteuzi wake, Jaji Sacko ametangaza azma ya kushughulikia ukiukaji wa haki za binadamu katika bara la Afrika. “Nitahakikisha nawasiliana na viongozi na mamlaka za haki ili kupunguza ukiukwaji wa haki za binadamu,” amesema.
Aidha, Jaji Bensaoula Chafika wa Algeria ameteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Mahakama hiyo.
Changamoto kuu itakayoathiri kazi ya mahakama ni uhitaji wa nchi za Afrika kutekeleza hukumu zilizotolewa, jambo ambalo litahitaji ushirikiano mkubwa kati ya nchi na taasisi ya haki.