Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko Aielekeza Kupunguza Upotevu wa Maji
Dk. Biteko amesema jijini Dar es Salaam kuwa upatikanaji wa huduma za maji ni haki ya msingi, na kwa hivyo lazima kulinda vyanzo vya maji ili kuwezesha upatikanaji wake.
Akizungumza wakati wa kuzindua ripoti ya utendaji wa mamlaka za maji kwa mwaka 2023/24, Biteko ameeleza kuwa jamii ina wajibu wa kuhakikisha usafi wa mazingira, kupanda miti na kuhifadhi misitu ili kuendelea kupata na kutumia rasilimali maji.
“Tusipotunza vyanzo vya maji na kuhifadhi mazingira, tutajikuta katika mtanziko mkubwa wa ukosefu wa maji,” alisema. Ameonyesha kuwa ukosefu wa rasilimali maji kunaweza kuwa chanzo cha migogoro na machafuko katika jamii.
Ripoti ilizungumzia kuwa asilimia 84 ya maeneo ya mijini na asilimia 79.6 ya maeneo ya vijijini sasa zimeshauganishwa na huduma ya maji, ikionesha ongezeko la asilimia 7 ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Mamlaka zenye utendaji bora katika kudhibiti upotevu wa maji ni pamoja na Maganzo (4%), Nzega (6%), na Kashuwasa (11%). Hata hivyo, baadhi ya mamlaka kama vile Rombo (70%) na Handeni (69%) bado znahitaji kuboresha utendaji wao.
Dk. Biteko alizungumzia kuwa lengo kuu ni kupunguza hasara ya takriban sh 114.12 bilioni zilizotokana na upotevu wa maji, na kuhakikisha upatikanaji wa maji salama kwa wakazi wote.