SHILINGI BILIONI 25 ZITENGWA KUIMARISHA MAZINGIRA NA USTAWI WA JAMII
Serikali imetangaza utekelezaji wa mradi muhimu wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bayoanuai Tanzania, kwa lengo la kuboresha hali ya mazingira na kuimarisha maisha ya wananchi.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kiasi cha Shilingi Bilioni 25 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo ambao unasimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Mradi unaojumuisha Mikoa 5 na Halmashauri 7 unalenga kuboresha uhifadhi wa mazingira, kuwezesha jamii kupata kipato na kuchangia maendeleo endelevu.
“Tumepanga kuongeza maeneo ya utekelezaji kufikia jamii zaidi nchini,” alisema Luhemeja. Ameeleza kuwa wananchi wamefurahishwa na mradi, akizitaka jamii kuendelea kuhifadhi mazingira na kubuni miradi shirikishi.
Kwa sasa, mradi umefafikia kiwango cha asilimia 67 na unatarajia kukamilika mwaka 2025, ikiwemo kujenga uwezo wa jamii katika miradi ya mazingira na kiuchumi.
Mbinu kama vile kilimo rafiki mazingira na biashara ya kaboni zimewezesha wananchi kupata mapato zaidi na kuboresha mazingira yao.