BREAKING: Mshukiwa Akamatwa kwa Kuanzisha Kituo Cha Polisi Isiyo Halali
Mtu mmoja, Collins Leitich, mkaazi wa Kaunti ya Uasin Gishu, amekamatwa na mamlaka za usalama kwa kosa la kuanzisha na kuendesha kituo cha polisi isiyo rasmi.
Leitich alipaka kituo hicho rangi ya polisi ili lionekane halali, jambo ambalo lilishangaza mamlaka za eneo husika. Maafisa wa usalama walimkamata mshukiwa juzi tarehe 8 Machi.
Wakazi wa eneo hilo walionyesha mchanganyiko wa mawazo, baadhi wakipongeza juhudi zake za kuboresha usalama, wakati wengine wakishangaa na vitendo vya mshukiwa.
Mamlaka zinachunguza kwa kina kiasi cha muda ambao kituo hicho kilikuwa kinaendesha, pamoja na kuchunguza ikiwa maofisa wa polisi au wakazi walikuwa wamefahamu uwepo wake.
Kwa mujibu wa sheria ya Huduma ya Polisi ya Kitaifa ya mwaka 2014, pekee Inspekta Jenerali wa Polisi ana mamlaka ya kuanzisha vituo rasmi vya polisi, ambavyo lazima viambatanishwe kwa usawa katika kaunti zote.
Uchunguzi unaendelea ili kubainisha undani wa jambo hili.