HABARI KUBWA: HALI YA KIAFYA YA PAPA FRANCIS INAANZA KUIMARIKA
Roma – Afya ya Papa Francis (88) inaonyesha ishara nzuri ya kuboresha, kwa mujibu wa taarifa rasmi zilizotolewa. Hivi karibuni, kiongozi wa kimataifa wa Kanisa Katoliki alikuwa amehudumu hospitalini akipatiwa matibabu ya nimonia.
Taarifa ya siku ya Jumanne, Februari 25, 2025 inathibitisha kuwa hali yake ya kiafya, ingawa bado ni mahututi, inaonyesha alama ya kuboresha. Vipimo vya maabara vimeashiria maboresho ya mwitiko wa matibabu.
Papa Francis amekuwa akipatiwa matibabu hospitalini ya Gemelli mjini Roma siku ya 12, na hivi sasa hali yake inaanza kuimarika tofauti na siku zilizopita. Mwanzo, Vatican ilitangaza kuwa hali yake ilikuwa mbaya, akiwekwa chumba cha uangalizi maalumu akipumua kwa msaada wa mashine.
Hata hivyo, Vatican imebainisha kuwa Francis bado anaweza kusogea, si mgonjwa kitandani na anakala vizuri. Pia ameendelea na baadhi ya majukumu yake, ikijumuisha kupokea Ekaristi na kuendelea na kazi zake za kawaida.
Waumini na viongozi wa kidini duniani kote wamekusanyika kumuombea, huku familia yake ikiwa na wasiwasi. Binamu wake Carla Rabezzana alisisitiza umuhimu wa kutumaini na kuomba kwa ajili ya afya yake.
Madaktari wanasema kuwa hali ya figo ya Papa Francis inaonekana kuwa ya muda mfupi na inaweza kuboresha kwa matibabu sahihi. Hata hivyo, wanashauri kuwa umri wake wake unahitaji tahadhari zaidi.
Jambo la kushangaza ni kuwa Papa Francis ameendelea kuwa msimamo wa utulivu na kuimarika, hata katika hali ngumu ya kiafya.