WANAHARAKATI wa Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira wamewashauri viongozi wakuu wa Afrika kuzingatia teknolojia ya nishati jadidifu na endelevu katika utekelezaji wa mpango wa kuwafikishia umeme waafrika milioni 300 ikifapo mwaka 2030.
Wanaharakati hao wametoa wito kwa Serikali za nchi za Afrika kulingana na fedha zilizotengwa kuhakikisha wanatoa kipaombele katika nishati jadidifu kama vile uzalishaji wa umeme wa maji, jua, upepo na joto ardhi.
Mratibu wa taasisi ya TNC Tanzania, amesema endapo Serikali itajikita katika kuwekeza katika nishati hizo jadidifu, itapunguza kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi.
“Umeme ni nyenzo kubwa sana ya maisha ya binadamu, kwa hiyo basi tulikuwa na mapendekezo yetu ya kuiambia Serikali kwamba wawekeze katika kwenye nishati safi ambayo ni nishati ya jua, nishati ya upepo, nishati joto ardhi na nishati ya maji,” ameeleza mratibu.
Katika mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika, umefanikiwa kupata ahadi za ufadhili wa Dola za Marekani Bilioni 40 kwa ajili ya kuwezesha usambazaji wa umeme barani Afrika. Jumla ya nchi za Afrika 12 zimeingia kwenye Mipango Mahsusi wa Kitaifa kuhusu Nishati.
Rais wa Tanzania alisema Mpango Mahsusi wa Kitaifa kuhusu Nishati unalenga kuiwezesha Tanzania kuunganisha umeme kwa kaya milioni 8.3 zaidi ifikapo mwaka 2030.
Wanaharakati wanasikitisha changamoto za mazingira na wanawaomba viongozi kuhakikisha teknolojia safi na endelevu inatumiwa ili kuwalinda vizazi vijavyo na kuimarisha uchumi wa nchi.