Saturday, March 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Tanzania yajizatiti teknolojia ya mawasiliano angani

by TNC
January 24, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Dar es Salaam. Wakati uhakika wa mawasiliano ya anga ukitajwa kuchochea ndege za kimataifa kupita Tanzania kuongeza mapato, Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imesema matumizi ya teknolojia za kisasa yanachangia uhakika huo pamoja na kuepusha ajali angani.

Teknolojia hizo ikiwemo ile ya mifumo mipya ya mawasiliano kati ya rubani na waongozaji wa ndege kupitia redio za mawasiliano (VHF-Digital radio), reda, pamoja na teknolojia za kutoa taarifa za hali ya hewa kila baada ya nusu saa.

Hayo yamebainishwa Januari 23, 2026 na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Salim Msangi ambaye amesema teknolojia katika mawasiliano ya anga ndio usalama wa anga, hivyo haikwepeki.

Amesema hayo alipofungua mkutano wa 45 wa mwaka wa Chama cha Waongoza Ndege Nchini (TATCA), uliofanyika Januari 23, 2026 jijini Dar es Salaam.

"Tumejizatiti uhakika wa mawasiliano ya anga ya kisasa kwa kuwa ndio usalama wa anga. Ndege zisipowasiliana angani na waongoza ndege, uwezekani wa kupata ajali ni mkubwa. Sisi kwenye hili tumejizatiti vizuri hatuna ajali inayotokana na kukosa mawasiliano," amesema.

Mkurugenzi huyo mkuu amesema kufungwa kwa mifumo hiyo kunafanya ndege ziweze kuwasiliana kama inavyotakiwa katika ubora wa kimataifa.

Akizungumzia changamoto, amesema teknolojia zinabadilika mara kwa mara na pia ni gharama. Pia, wataalamu wa sekta ya uongozaji ndege ni changamoto kuwapata ukizingatia na mafunzo yao ni gharama.

Akieleza zaidi amesema, chama hicho malengo yake ni pamoja na kuimarisha usalama, ufanisi, na taratibu za urubani wa anga kitaifa na kimataifa.

Kadhalika, kutoa msaada na ushauri katika uendelezaji wa mifumo salama na yenye mpangilio wa uongozi wa ndege, na kukuza viwango vya juu vya maarifa na taaluma miongoni mwa waongoza ndege.

"Hii ni fursa muhimu kuwahakikishia kuwa tutaendelea kushirikiana na taasisi yenu ili kufikia malengo yote matatu niliyoyataja, na hivyo kuongeza usalama na uhakika wa safari za anga ndani ya anga la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," amesema.

Rais wa TATCA, Merkiory Ndaboya akizungumza kuhusu mkutano huo uliowakutanisha na wadau kutoka nje ya Tanzania amesema wanatumia akili unde (AI) kuwasaidia katika kutelekeza majukumu.

"Pia, ipo mitambo ya kisasa, teknolojia ya reda ambayo inajua ndege iko umbali gani ipo na spidi gani. Teknolojia ya rubani kupata taarifa, mitambo ya kupeleka taarifa kwenye kompyuta kuhusu uelekeo na spidi ya upepo," amesema.

Kwa upande wake, muongoza ndege kutoka Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Hellen Mosha amesema watatumia mkutano huo kujadili mambo mbalimbali yanayowakabili katika sekta yao.

"Tunahakikisha tunakwenda sambamba na teknolojia," amesema Hellen.

Tags: AnganiMawasilianoTanzaniaTeknolojiayajizatiti
TNC

TNC

Next Post

Zanzibar yaanza hatua mpya kuelekea uchimbaji wa mafuta na gesi asilia

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company