Saturday, March 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Sh249 milioni kuboresha zahanati ya shule ya mahitaji maalumu

by TNC
January 24, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Halmashauri ya Rungwe Yatumia Sh249 Milioni Kuboresha Zahanati ya Shule ya Mahitaji Maalumu

Rungwe. Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya imetumia zaidi ya shilingi milioni 249 kuboresha miundombinu ya zahanati katika Shule ya Msingi Katumba II Mchanganyiko.

Shule hiyo inayohudumia wanafunzi wenye mahitaji maalumu, imepewa fedha hizo kuweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa huduma bora za afya kwa kundi hilo.

Hatua hiyo imeelezwa kuwa mwarobaini wa changamoto za kiafya zinazowakabili wanafunzi wenye ulemavu wa viungo vya aina mbalimbali, ambao huhitaji huduma za karibu na rafiki kulingana na hali zao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Renatus Mchau, amesema fedha hizo zimetolewa na Serikali Kuu kutokana na umaalumu wa shule hiyo na mahitaji ya wanafunzi wanaoisoma.

Amesema pamoja na ukarabati wa zahanati, Serikali pia hutoa zaidi ya shilingi milioni 14 kila mwezi kwa ajili ya kugharamia mahitaji mbalimbali ya shule hiyo ikiwemo chakula cha wanafunzi.

"Serikali kila mwezi inatoa shilingi milioni 14 kusaidia mahitaji ya shule. Hata hivyo, bado kuna changamoto ya baadhi ya wazazi kutorejea kuwachukua watoto wao wakati wa likizo, jambo linaloongeza mzigo kwa walimu na uongozi wa shule," amesema Mchau.

Ameeleza kuwa maboresho ya zahanati hiyo yanaambatana na ujenzi wa jengo la mapokezi, nyumba ya mtumishi na vyoo, ili kuhakikisha huduma za afya zinapatikana kwa viwango vinavyokidhi mahitaji ya wanafunzi na jamii inayozunguka shule hiyo.

Mchau ameishukuru Serikali Kuu kwa kuendelea kuitupia jicho Shule ya Katumba II Mchanganyiko yenye zaidi ya wanafunzi 250 wenye mahitaji maalum, akisema uwekezaji huo utapunguza usumbufu kwa walimu na wanafunzi endapo kutatokea dharura za kiafya.

"Pamoja na idadi kubwa ya wanafunzi, halmashauri inatenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu, ikiwemo ujenzi wa bweni lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 80, kwa lengo la kuongeza wigo wa huduma," amesema.

Uwekezaji wa Elimu Unaendelea

Kaimu Ofisa Elimu Awali na Msingi Wilaya ya Rungwe, Kotasi Mbwilo, amesema Serikali itaendelea kuwekeza katika miundombinu ya Shule ya Katumba II na shule nyingine, ili kuwawezesha watoto wenye mahitaji maalum kutimiza ndoto zao za kupata elimu bora.

Amesema halmashauri ina jumla ya shule za msingi 160, zikiwemo 10 binafsi, huku akibainisha kuwa katika kipindi cha miaka miwili shule tatu mpya zimefunguliwa na vyumba vya madarasa kuongezeka kutoka 1,157 hadi 1,195.

Mbwilo ameongeza kuwa halmashauri imepokea shilingi milioni 659 kupitia mradi wa BOOST kwa ajili ya ujenzi wa shule mbili mpya katika maeneo ya Ndaga (Kata ya Ndanto) na Kisa (Kata ya Kisondelo).

Mkazi wa Msasani wilayani Rungwe, Ester John, ameipongeza Serikali kwa maboresho makubwa katika sekta ya elimu, akisema miundombinu rafiki imeongeza hamasa ya wazazi kuwapeleka watoto shule.

"Tunaona miundombinu sekta ya elimu hususani shikizi na mahitaji maalum zikijengwa kwa viwango vya hali ya juu jambo ambalo kama wazazi sada tunaona umuhimu wa elimu kwa watoto," amesema.

Tags: kuboreshamaalumuMahitajiMilioniSh249Shulezahanati
TNC

TNC

Next Post

Final message of party founder and first central bank Governor Mtei to his family

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company