Sunday, March 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Njaa kuhatarisha masoko na utulivu duniani

by TNC
January 20, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Njaa Inahatarisha Utulivu wa Dunia, WFP Yaonya Davos

Dar es Salaam – Wakati viongozi wa dunia wakikutana katika Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) huko Davos, Uswisi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeonya kuwa kushindwa kukabiliana na njaa kunahatarisha maisha ya watu, masoko na utulivu duniani.

Onyo hilo la WFP limetolewa Jumatatu Januari 20, 2026 katika mkutano huo unaowakutanisha viongozi mbalimbali, wataalamu, sekta binafsi na wadau wengine wanaowakilisha mataifa yao.

WFP imebainisha kuwa watu milioni 318 duniani wanakabiliwa na njaa mwaka huu huku wengi wakipata chakula kisichotosheleza mahitaji. Shirika hilo linafanya kazi kwa chini ya nusu ya bajeti inayohitajika ya dola bilioni 13, hali inayolazimisha kupunguza mgao wa chakula kwa mamilioni ya watu wenye uhitaji.

Rania Dagash-Kamara, Mkurugenzi Mtendaji Msaidizi wa WFP anayeshughulikia Ushirikiano na Ubunifu, amesema dunia haiwezi kujenga masoko thabiti katika hali ambayo zaidi ya watu milioni 318 wanakabiliwa na njaa.

Kamara amesisitiza kuwa njaa husababisha migogoro na ukosefu wa utulivu na haya yote yanavuruga masoko ambayo biashara zinayategemea, akionya kuwa bila uwekezaji wa haraka, athari zitakuwa mbaya zaidi.

Pengo la Ufadhili Lazima Tiba

Shirika hilo la kushughulikia masuala ya chakula linasema pengo la ufadhili linalifanya kuwa na uwezo wa kuwafikia takribani theluthi moja tu ya walio katika uhitaji mkubwa zaidi wa msaaada wa chakula duniani.

Katika kipindi ambacho rasilimali za umma kwa mashirika ya kibinadamu zinapungua, WFP inasema ushirikiano na sekta binafsi unazidi kuwa muhimu zaidi katika kukabiliana na umasikini na kuleta usawa wa kiuchumi duniani.

Utajiri wa Mabilionea Umeongezeka

Mbali na janga la njaa, utafiti umeonyesha kuwa utajiri wa mabilionea umeendelea kuongezeka kwa kasi, huku mabilioni ya watu wakikabiliwa na kushuka kwa kipato na kupanda kwa gharama za maisha.

Takriban mabilionea 3,000 duniani walikuwa na utajiri wa jumla wa dola trilioni 18.3 mwaka jana. Licha ya mfumuko wa bei, utajiri wao umeongezeka kwa zaidi ya asilimia 80 tangu Machi 2020 huku karibu nusu ya idadi ya watu duniani wakiendelea kuishi katika umaskini.

Zaidi ya watu bilioni nne duniani wanaishi katika umasikini, ni sawa na kusema mtu mmoja katika kila watu wanne hawezi kumudu gharama muhimu za kila siku.

Vikao vya WEF 2026

WEF, iliyoanzishwa mwaka 1971, imeendelea kuwa jukwaa muhimu la kuwakutanisha viongozi wa serikali, sekta binafsi, wataalamu na asasi za kiraia.

WEF 2026 limebeba uzito wa kipekee kwa sababu limekuja wakati dunia ikipitia migogoro ya kiuchumi na kisiasa inayoendelea duniani, likizikutanisha nchi zaidi ya 200 na washiriki zaidi ya 3,000, huko Uswisi.

Jukwaa hilo linaendelea kujadili mada mbalimbali za kiuchumi duniani huku likitarajia kuhitimisha vikao vyake, Jumamosi Januari 24, 2026.

Tags: DunianikuhatarishamasokoNjaaUtulivu
TNC

TNC

Next Post

Tanzania addresses limited knowledge of international scholarship opportunities

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company