Saturday, March 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Mwasisi wa chama cha siasa afariki dunia

by TNC
January 20, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Arusha. Mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edwin Mtei, na aliyekuwa Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), amefariki dunia.

Mzee Mtei (94) ambaye alikuwa Gavana wa BoT kuanzia 1966 na miaka 12 baadaye akaja kuwa Waziri wa Fedha na Mipango amefariki usiku wa kuamkia leo Januari 20, 2025.

Ameitumikia nafasi ya Waziri wa Fedha na Mipango kuanzia 1978 mpaka 1981 alipojiuzulu wadhifa huo.

TNC imebaini kuwa Mzee Mtei aliugua kwa kipindi kirefu na hali yake ilibadilika ghafla wakati anapelekwa hospitali ya Seliani, akifariki njiani kabla ya kufika hospitalini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa, John Heche, chama hicho kimepoteza moja ya nguzo imara sana.

"Chama chetu kitatoa taarifa rasmi ya asubuhi. Tunachukua nafasi hii kutoa pole sana kwa familia ya mzee Mtei, ndugu jamaa na marafiki," amesema Heche.

"Chadema tumepoteza moja ya nguzo imara sana za chama chetu. Tutamuenzi Mzee Mtei kwa mema yote aliyoyafanya kwa chama na nchi yetu."

Mzee Mtei aliasisi Chama cha Chadema mwaka 1992 na kuwa mwenyekiti wake wa kwanza ambapo amefariki dunia chama kikiwa kinaadhimisha miaka 33 tangu kipewe usajili.

Mzee Mtei alizaliwa Julai 12, 1932 Marangu, Moshi mkoani Kilimanjaro. Kwa sasa msiba uko nyumbani kwake Tengeru, Arusha ambapo mipango ya mazishi inafanyika.

Tags: afarikichaChamaduniaMwasisisiasa
TNC

TNC

Next Post

Tanzania mguu sawa uwekezaji sayansi ya bahari

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company