Saturday, March 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Waimbaji wa ngoma za kiasili wazindua sakata la uuzaji wa muziki

by TNC
January 19, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

ACT-Wazalendo na SMZ Wazidi Kuvutana Kuhusu Kuingia SUK

Dar es Salaam. Ugumu umeendelea kuyatawala mazungumzo kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Chama cha ACT-Wazalendo kuhusu mwafaka wa chama hicho kuingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Hii inakuja baada ya ACT-Wazalendo kuweka wazi kuwa haijaafikiana na Serikali kuingia SUK, kwa sababu Serikali ya Zanzibar haijajibu matakwa yao.

ACT-Wazalendo imekuja na msimamo huo, wakati Jumapili Januari 18, 2026 ndio iliyotarajiwa kuwa siku ambayo kingetoa kauli ya kuingia SUK, baada ya mvutano wa takriban mwezi mmoja na Serikali ya Zanzibar.

Hali imeendelea kuwa ngumu, ingawa zimesalia siku 22 kati ya zile 90 ambazo kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, ACT-Wazalendo iliyopata zaidi ya asilimia 10 ya kura za Rais wa Zanzibar inapaswa kuingia SUK.

Hata hivyo, Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi, alipoteua Baraza la Mawaziri, aliacha nafasi nne zitakazozibwa na wajumbe kutoka chama hicho kikuu cha upinzani.

TNC imezungumza na wajumbe kadhaa wa kamati kuu waliokuwa sehemu ya kikao hicho, wamesema hakuna mwafaka uliofikiwa, hivyo bado hakijaeleweka kuhusu chama hicho kuingia SUK.

Kwa mujibu wa viongozi hao walioomba hifadhi ya majina yao, kutofikiwa kwa mwafaka huo kumetokana na Serikali kutotimiza matakwa ya chama hicho, ambayo hata hivyo hawajayaweka wazi.

"Bado hawajajibu matakwa yetu. ACT-Wazalendo bado tunavutana na Serikali kuhusu kuingia SUK," amesema kiongozi huyo aliyekuwa katika kikao hicho cha kamati kuu.

Hadi saa 12:15 jioni, bado kikao hicho kilikuwa kinaendelea, lakini msimamo wa chama hicho hadi muda huo ni kwamba hawataingia SUK hadi matakwa yao yatakapotimizwa.

Historia ya Mvutano

Mvutano wa ACT-Wazalendo na Serikali ya Zanzibar kuingia katika SUK ulianza mapema Novemba mwaka jana, baada ya Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar, Balozi Zena Ahmed Said kukiandikia barua chama hicho ili kipeleke jina la Makamu wa Kwanza wa Rais.

Hata hivyo, Novemba 13, 2025, Mwenyekiti wa chama hicho, Othman Masoud Othman aliwaambia wanachama akiwa ziarani Pemba visiwani humo kuwa hawakupeleka jina wakati huo, kwa madai ya kutoridhishwa na mazingira ya kisiasa.

Baada ya mvutano huo, chama hicho kilipanga kikao cha kamati kuu kilichofanyika Januari 17 na 18 mwaka huu, kujadili pamoja na mambo mengine, uamuzi wa mwisho kuhusu ama kuingia SUK au vinginevyo.

Lakini kikao hicho si cha kwanza, kamati ya uongozi ya chama hicho ilishaketi Novemba 23 mwaka jana visiwani Zanzibar kutathmini kuhusu uchaguzi na iligusia suala la SUK, ingawa sio kwa mapana yake.

Masharti ya ACT-Wazalendo

Mapema mwezi huu, TNC ilizungumza na mmoja kati ya viongozi wa chama hicho aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema ACT-Wazalendo imeweka masharti kadhaa ili kuingia SUK na baadhi inadaiwa yameshaanza kutekelezwa, ingawa hajayaweka wazi.

Kwa sababu hiyo, kiongozi huyo alisema inakifanya chama hicho kitangulize mguu mmoja ndani ya SUK, huku jitihada nyingine zikiendelea kuhakikisha mwafaka baina ya pande zote unafikiwa.

Hata hivyo, alieleza kumekuwa na juhudi za kila namna zinazofanywa na Serikali ya Zanzibar kuishawishi ACT-Wazalendo iingie SUK ikiwamo kuwatumia wazee maarufu wa Bara na Zanzibar na watu wengine maarufu.

Pia, alisema wapo viongozi wasiotaka kabisa chama hicho kiingie SUK kwa sababu wanadai walidhulumiwa uchaguzi, hivyo ziendelee juhudi za kudai haki.

Alisema chama hicho kimefungua kesi mbalimbali za uchaguzi kushinikiza kupatikana kwa haki zake, wakati huo huo kimeshatanguliza mguu kuingia SUK, bila kuathiri mapambano ya kudai haki.

Msimamo wa ACT-Wazalendo

Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Bara, Issihaka Mchinjita alisema msimamo wao ni kwamba, kabla ya kuingia au kutoingia, wanaangalia iwapo kwa mazingira yaliyopo sasa malengo ya kuanzishwa SUK yatafikiwa.

Alieleza SUK ilianzishwa kuepusha mitafaruku na migogoro ya kisiasa na kijamii, uhasama wa kiraia na kinachofanywa na ACT-Wazalendo ni kutathmini iwapo hatua yao ya kuingia mwaka 2020 imeleta matokeo chanya.

Kwa tathmini yao, alisema wanaona pamoja na chama hicho kuingia SUK 2020, hakuna matokeo chanya yaliyopatikana, hivyo wanatafakari kuona je, wanapaswa kuingia kwa namna ile ile au kwa namna ipi itakayoleta tija kwa umma.

"Tunaona kuingia kwa namna tulivyoingia hatuoni malengo ya kuanzishwa kwa SUK yakitimia. Ikiwa kuingia kwa namna ya zamani itakuwa muarobaini tutaingia, lakini ikiwa kuingia ni kwa sababu ya kupeana vyeo haitakuwa na maana," alisema Mchinjita.

"Tuko tayari kujadiliana kwenye eneo hilo na zipo hatua zinazochukuliwa ingawa ni za ndani kwa sasa, tunatazama na kuona kama itafika hatua ya kutoa taarifa kwa umma."

"Suala la SUK ni moja ya mambo ambayo kamati kuu itapokea taarifa yake na kutoa mwongozo. Kikao hicho pia kitafanya tathmini ya jumla ya masuala ya uchaguzi," aliongeza.

Tags: kiasilimuzikingomaSakataUuzajiWaimbajiWazindua
TNC

TNC

Next Post

How digital tools will define 2050 as players meet

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company