Saturday, March 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

RC Macha ashtakiwa kwa rushwa baada ya mchezo

by TNC
January 16, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Maswa – Wanafunzi wasio na sare mkoani Simiyu hawapaswi kuzuiwa kuhudhuria masomo hasa wale wa darasa la kwanza kwa shule za msingi na kidato cha kwanza kwa shule za sekondari, kwani kufanya hivyo ni kuwanyima haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha wakati wa ziara yake wilayani Maswa kukagua mahudhurio ya wanafunzi katika shule ya msingi Shanwa na shule za sekondari za Zanzui, Binza na Nyalikungu zilizopo wilayani humo.

Katika ziara hiyo Macha amebaini kuwa idadi kubwa ya wanafunzi wa darasa la kwanza na kidato cha kwanza hawajaripoti shuleni tangu kufunguliwa kwa muhula wa masomo Januari 13, 2025 huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni kukosa sare za shule.

Amesema kuwa kukosa sare hakupaswi kuwa kikwazo cha mtoto kupata elimu, akiwataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto shule mara moja hata kama bado hawajakamilisha mahitaji hayo.

"Wanafunzi wote wanaopaswa kuanza darasa la kwanza na wale wa kidato cha kwanza ambao hawana sare na hata mahitaji mengine ya shule wanapaswa kuwepo madarasani na kuanza masomo huku wazazi na walezi wakiendelea kukamilisha mahitaji yao," amesema.

Macha ametangaza kuwa kuanzia Januari 19, 2025, mkoa huo utaanza msako wa nyumba kwa nyumba kuwasaka wanafunzi wote ambao hawajaripoti shuleni, hatua hiyo inalenga kuhakikisha hakuna mtoto anayebaki nyumbani bila sababu za msingi.

Katika Shule ya sekondari Zanzui, Macha aliguswa na hali ya mwanafunzi Mary Charles, anayesoma kidato cha kwanza ambaye aliendelea kuhudhuria masomo bila sare ya shule kutokana na moyo huo wa bidii. Aliahidi kumnunulia mwanafunzi huyo sare za shule pamoja na madaftari kama motisha ya kuendelea na masomo.

Akizungumzia hali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dk Vicent Anney amesema kuwa serikali haitamvumilia mzazi au mlezi anayemzuia mtoto kwenda shule kwa makusudi.

"Hakuna mzazi atakayekuwa na sababu ya kumzuia mtoto kwenda shule kwa kisingizio cha sare. Mtoto anatakiwa awe darasani kwanza, sare zitafuata. Elimu ni haki ya msingi ya mtoto," amesema.

Juma Shija ni mkazi wa kijiji cha Zanzui amesema kuwa hatua hiyo itasaidia watoto wengi waliokuwa wakibaki nyumbani.

"Wazazi wengi walikuwa wanaona aibu kuwapeleka watoto shule bila sare, sasa kauli hii imetupa mwanga. Mtoto bora asome kuliko akae nyumbani," amesema.

Kwa upande wake, Esther John ni mzazi wa mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Nyalikungu iliyopo wilayani humo amesema kuwa uamuzi huo ni mzuri na utatoa nafasi kwa watoto kupata elimu.

"Huu ni uamuzi mzuri sana. Hali ya maisha ni ngumu, lakini mtoto hapaswi kuathirika. Tumeanza tayari kuwapeleka watoto wetu shule," amesema.

Naye Paulo Ng’wala ambaye ni mkazi wa Maswa mjini, aliipongeza serikali kwa kuchukua hatua za ufuatiliaji.

"Msako wa nyumba kwa nyumba utawafanya wazazi wazembe wawajibike. Elimu ndiyo urithi pekee wa mtoto maskini," amesema.

Tags: AshtakiwaBaadakwaMachamchezoRushwa
TNC

TNC

Next Post

Mandawa anaposahau kumbakishia Mstaafu

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company