Saturday, March 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Uchaguzi mkuu kufanyika ‘gizani’ Uganda unahojiwa

by TNC
January 15, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Uganda: UN Ihoji Kuzimwa Kwa Mitandao Wakati wa Uchaguzi Mkuu

Kampala – Umoja wa Mataifa (UN) kupitia Ofisi ya Haki za Binadamu umehoji kuzimwa mitandao na kuitaka Uganda kuondoa marufuku kuzima intaneti, ikisema hatua hiyo inaiweka nchi ‘gizani’ kwa kukosekana mawasiliano na uwazi wakati uchaguzi mkuu ukifanyika leo Alhamisi.

Ofisi ya Haki za Binadamu ya UN imesisitiza kupitia ujumbe wa mitandao ya kijamii uliochapishwa Jumatano Januari 14, 2026 ikieleza kuwa upatikanaji wazi wa mawasiliano na taarifa ni muhimu kwa uchaguzi huru na wa kweli.

"Waganda wote lazima waweze kushiriki katika kuunda mustakabali wao na mustakabali wa nchi yao," ilieleza taarifa hiyo.

Utekelezaji wa agizo kukatwa intaneti ulianza Jumanne jioni baada ya Tume ya Mawasiliano ya Uganda (UCC) kuwaagiza waendeshaji wa mitandao ya simu kuzuia upatikanaji wa intaneti kwa umma.

Taasisi ya ufuatiliaji wa intaneti imesema hatua hiyo inaweza kupunguza uwazi na kuongeza hatari ya udanganyifu wa kura.

UN pia imetahadharisha kwamba huenda Waganda wakapiga kura katika mazingira ya ukandamizaji na vitisho dhidi ya upinzani wa kisiasa, watetezi wa haki za binadamu, waandishi wa habari na wale wenye maoni ya kupinga.

Tume ya Mawasiliano ya Uganda imetetea hatua ya kuzima intaneti ikisema ni muhimu kudhibiti taarifa za upotoshaji, udanganyifu wa kubaini na kuzuia vurugu zinazohusiana na uchaguzi mkuu.

Wataalam wa haki za binadamu wametaja hatua ya kuzimwa kwa intaneti kuwa ni shambulio la wazi dhidi ya haki ya uhuru wa kujieleza, wakibainisha athari zake kubwa kwa uhuru wa kusafiri, maisha ya watu, na upatikanaji wa taarifa.

Rais Yoweri Museveni, mwenye umri wa miaka 81, anakabiliwa na upinzani kutoka kwa mwanasiasa Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine, huku kukiwa na wagombea wengine sita wanaowania nafasi hiyo.

Tags: gizanikufanyikaMkuuuchaguziUgandaunahojiwa
TNC

TNC

Next Post

What the general election outcome means for a neighboring country

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company