Saturday, March 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Trump atangaza mpango wa mafuta Venezuela

by TNC
January 10, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Trump Azidi Kusisitiza Udhibiti wa Greenland, Asema ni Suala la Usalama wa Taifa

Marekani. Rais Donald Trump wa Marekani amerejea tena kauli yake ya kutaka nchi yake ichukue udhibiti wa eneo la Greenland, akisema hatua hiyo ni muhimu kwa maslahi ya usalama wa taifa.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa mkutano mrefu uliofanyikia Ikulu ya White House na wakuu wa kampuni za mafuta kuhusu uwekezaji nchini Venezuela Januari 9, 2026.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano huo, Trump amesema ana matumaini ya kufikia makubaliano na Serikali ya Denmark kuhusu Greenland, eneo lenye mamlaka ya kujitawala, akisisitiza kuwa umiliki kamili ni muhimu kuliko makubaliano ya muda mrefu ya kijeshi.

"Nchi lazima iwe na umiliki ndipo iweze kujilinda. Huwezi kulinda mikataba ya upangaji," amesema Trump, akiongeza kuwa endapo Marekani haitachukua hatua, basi China au Russia zinaweza kufanya hivyo.

"Sitaki China au Russia wawe majirani zangu Greenland. Hilo halitatokea," amesisitiza.

Kauli hizo zimekuja sambamba na mjadala mpana kuhusu mustakabali wa sekta ya mafuta ya Venezuela, chini ya uongozi mpya baada ya kukamatwa kwa rais wa zamani wa nchi hiyo kwa tuhuma za kula njama ya biashara ya dawa za kulevya, tukio lililotokea chini ya wiki moja iliyopita.

Marekani Yadhibiti Uwekezaji wa Mafuta Venezuela

Trump amesema Marekani itatoa dhamana za kiusalama kwa kampuni za Marekani zitakazowekeza Venezuela, akitaja hofu ya mashambulizi dhidi ya kampuni hizo.

Amefichua kuwa meli nyingi za kivita za Marekani zilizopo karibu na pwani ya Venezuela zitatumika kulinda maslahi ya Marekani.

Kwa mujibu wa rais huyo, ni Marekani itakayoamua ni kampuni zipi zitaruhusiwa kufanya kazi nchini Venezuela, akiongeza kuwa chini ya uongozi mpya, nchi hiyo inaelekea kuwa mshirika wa karibu wa Marekani.

Kuhusu mapato ya mauzo ya mafuta, Trump amesema Venezuela itahudumiwa kwanza ili iweze kujiendesha, kampuni za mafuta zilipwe gharama zao, na fedha zitakazosalia zitaelekezwa Marekani.

"Tutahakikisha Venezuela inapata kile inachohitaji kuishi. Baada ya hapo, kutakuwa na fedha nyingi zilizobaki na hizo zitakwenda Marekani, na kampuni za mafuta zitafurahi," amesema.

Alipoulizwa kama kipaumbele chake Venezuela ni utulivu au demokrasia, Trump amesema kwa mtazamo wake mambo hayo ni karibu sawa.

"Tunataka utulivu, lakini pia tunataka demokrasia. Mwisho wa siku, itakuwa demokrasia," amejibu.

Trump pia ameonyesha kuwa yuko tayari kukutana na viongozi mbalimbali wa Venezuela, akiwemo kiongozi wa upinzani María Corina Machado, anayetarajiwa kuzuru Washington wiki ijayo.

Hata hivyo, hakuthibitisha kama Machado atapewa nafasi ya uongozi, akisema huenda "akashiriki kwa namna fulani."

Katika hatua nyingine, rais huyo amegusia maandamano yanayoendelea Iran, akisema anaunga mkono waandamanaji na kuonya kuwa Marekani inaweza kuingilia kati endapo ghasia zitaongezeka.

Kwa upande wa Greenland, wananchi wa eneo hilo wameeleza wasiwasi wao kuhusu kauli za Trump, wakisema wanataka kuachwa waamue mustakabali wao bila vitisho vya mataifa makubwa.

Tags: AtangazaMafutampangoTrumpVenezuela
TNC

TNC

Next Post

Mwinyi: Miundombinu ya elimu inakidhi mahitaji ya karne ya 21

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company