Sunday, March 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Wanu aelekeza Veta kusaka mapinduzi ya viwanda

by TNC
January 7, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Veta Ziagizwa Kuimarisha Ushirikiano na Sekta Binafsi

Moshi – Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir, ameelekeza vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi nchini (Veta) kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi ili kukuza ujuzi wa teknolojia mpya unaoendana na Mapinduzi ya Nne ya Viwanda.

Amesema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati mpana wa kuhakikisha vyuo vya Veta vinaendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia pamoja na mahitaji ya soko la ajira nchini.

Naibu Waziri Wanu amesema hayo leo, Januari 7, 2026, wakati alipotembelea Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Kilimanjaro (Veta Moshi), akisisitiza kuwa ni muhimu kuimarisha mafunzo yanayofaa ili vijana watakaohitimu wawe wamoja na teknolojia za kisasa na mahitaji halisi ya ajira.

"Ni muhimu Veta ihakikishe kuwa, ushirikiano huu unaimarishwa ili kuongeza ubora wa mafunzo, maelekezo yangu kwa uongozi wa Veta ni kuongeza wigo wa ushirikiano na makampuni mengi zaidi," amesema Wanu.

Aidha, amesisitiza utekelezaji wa mpango huo utafanyika kwa kuzingatia muelekeo wa Taifa uliowekwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050, pamoja na sera za sekta husika na miongozo mbalimbali ya kitaifa, ili kuhakikisha mikakati ya mafunzo ya Veta inalingana na malengo ya maendeleo ya nchi.

"Ninasisitiza kuwa ushirikiano baina ya Veta na sekta binafsi ujumuishe ukuzaji ujuzi katika teknolojia mpya na za kisasa zinazoendana na mapinduzi ya nne ya viwanda.

"Nimefarijika sana kujionea karakana za mafunzo zilizosheheni vifaa vya kisasa na vya thamani kubwa, hii inathibitisha kuwa chuo hiki ni cha kimkamati kinachochangia kuandaa nguvu kazi yenye ujuzi katika sekta za madini, uzalishaji viwandani na teknolojia ya kusafirisha mafuta na gesi kwa mfano katika mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP)," amesema Naibu Waziri huyo.

Mkuu wa chuo hicho, Lupakisyo Mapamba amesema chuo hicho kinaendelea kushirikiana na taasisi pamoja na makampuni mbalimbali katika kutoa mafunzo.

Aidha, amesema chuo hicho kinatoa bunifu mbalimbali kama majiko ya kutumia nishati safi na sufuria za kupikia jiko, na kwamba mafunzo wanayoyatoa yanatambulika Kitaifa.

Mbunge wa Moshi Mjini (CCM), Ibrahim Shayo amesema kutokana na ubunifu unaofanywa na chuo hicho atatoa ufadhili kwa vijana 10 kila mwaka ili kupata ujuzi mbalimbali katika chuo hicho zitakazowasaidia kujiajiri.

Tags: AelekezakusakaMapinduziVetaviwandaWanu
TNC

TNC

Next Post

Two foreign nationals charged with economic sabotage after Sh2bn uncovered in home

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company