Sunday, March 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

TaSUBa na Ubalozi wa India wawaibua wakali sanaa ya uchoraji

by TNC
January 2, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

TaSUBa Washindanisha Wanafunzi 20 Katika Sanaa ya Uchoraji

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kwa kushirikiana na ubalozi wa India, imewashindanisha wanafunzi 20 katika sanaa ya uchoraji iliyobeba mada kuu ya uhusiano wa Bahari wa Hindi na tamaduni za nchi ya Tanzania na India.

Mashindano hayo yaliyofanyika kwa siku tatu chuoni hapo ambapo washiriki walitakiwa kuonyesha uhusiano wa kiutamaduni uliopo kati ya nchi hizo na Bahari ya Hindi.

Akizungumza katika hitimisho la mashindano hayo, Naibu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri, Gabriel Kiiza amesema washindi watano wameteuliwa na kutunukiwa zawadi ya fedha taslimu.

"Katika mashindano hayo, wachoraji walitakiwa kuonyesha namna Bahari ya Hindi inavyounganisha tamaduni mbili za watu wa India na Tanzania," amesema Kiiza.

"Hivyo washindani waliweza kuchukua fikra zao, uzoefu na vitu mbalimbali vinavyowasilisha Watanzania na Wahindi."

Kiiza ameeleza kuwa wanafunzi waliohusika ni kuanzia ngazi ya cheti hadi shahada mwaka wa pili, na amekiri vipaji vya washiriki hao ni vizuri kwani wameweza kutafsiri kazi waliyopewa kwa kutumia vema vitendea kazi na muda waliopewa.

Changamoto za Sanaa ya Uchoraji

Kuhusu changamoto zilizopo katika sanaa ya uchoraji, Kiiza amesema ni pamoja na upatikanaji wa rangi na brashi ambazo nyingi kwa sasa zinatoka nje ya nchi.

Hata hivyo, pamoja na changamoto hiyo, amewataka vijana kuwa wabunifu kwa kutumia vitu vinavyopatikana katika mazingira yao kwani hiyo ndio sanaa yenyewe.

Ofisa Mwandamizi Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Jalala Sammatta, akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, amesema picha walizochora vijana zinapendeza na kudhihirisha kuwa wanachosomea wanakipenda.

Sammatta amesema sanaa ni maisha ya binadamu na kubwa ni uchumi, hivyo ni vema wanafunzi hao wakaandaliwa vizuri ambapo serikali kwa upande wake itaendelea kujitahidi kuwekeza hela katika tasnia hiyo.

Uhusiano wa Tanzania na India

"Pia mashindano hayo sio madogo kwani yanabeba taswira kubwa ya ushirikiano kati ya nchi ya India na Tanzania ambao umeanza miaka mingi iliyopita," amesema Sammatta.

"Wito kwa Watanzania kupenda vitu vya kwao vya sanaa kwa sababu wakifanya hivyo siyo tu wanaitangaza Tanzania na sanaa yake bali wanaimarisha uchumi kuanzia ngazi ya kaya."

Mwakilishi kutoka Ubalozi wa India, Lakshay Arand, amesema mashindano hayo ni wazo la kuihusisha Bahari ya Hindi na tamaduni za nchi hizo mbili katika mambo mbalimbali ikiwemo vyakula, lugha, masuala ya ulinzi na usalama.

Arand amesema katika uwasilishaji wa michoro hiyo wanafunzi wamejitahidi kuwasilisha mawazo yao na kueleza wanafurahia namna Tanzania imekuwa na ushirikiano wa karibu na nchi ya India katika masuala mbalimbali.

Mshindi Afichua Matarajio

Neema Labia, aliyeibuka mshindi wa kwanza katika mashindano hayo, amesema amejisikia vizuri kwa ushindi huo ukizingatia kulikuwa na ushindani mkubwa kwa wachoraji wenzake.

Neema amesema matarajio yake baada ya kumaliza chuo ni kuifanya kazi ya sanaa kuweza kuonekana zaidi kwani baadhi kwa sasa huona kama kuifanya ni kupoteza muda.

Tags: IndiasanaaTaSUBaUbaloziuchorajiwakaliwawaibua
TNC

TNC

Next Post

Bank dominates year-end stock exchange trading, commands 96pc of market turnover

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company