Saturday, March 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Makanisa wajipanga kuhudumia wafungwa 2026

by TNC
December 27, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Umoja wa Makanisa Kibaha Wapanga Kutoa Huduma Kwa Wafungwa Kuanzia 2026

Kibaha. Umoja wa Makanisa Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani umetangaza mpango wa kuanzia mwaka 2026 kuongeza nguvu katika utoaji wa huduma za kiroho na kijamii kwa wafungwa magerezani.

Umesema hatua hiyo inalenga kuwajenga kimaadili na kiroho, ili kupunguza vitendo vya uhalifu wanaporejea uraiani, sambamba na kuimarisha upendo, amani na mshikamano nchini.

Kupitia mpango huo, imeelezwa umoja huo utajikita katika kuwahubiria wafungwa neno la Mungu na kuwapatia mahitaji muhimu yasiyo katika bajeti ya Serikali, kama vile nguo, miswaki na sabuni kwa lengo la kuwafariji na kuwajengea moyo wa utu na matumaini mapya ya maisha bora baada ya vifungo.

Akizungumza Jumamosi, Desemba 27, 2025, wakati wa ibada ya Umoja wa Makanisa iliyofanyika Kibaha kwa lengo la kuliombea Taifa, Mwenyekiti wa umoja huo, Julius Shemkai amesema mpango huo unatokana na vitendo vya baadhi ya wafungwa wanaomaliza vifungo kurejea tena gerezani kwa makosa ya wizi na uporaji.

Amesema hiyo inasababishwa na baadhi yao kukosa maadili na hofu ya Mungu, jambo linaloonyesha umuhimu wa kuwaandaa wafungwa kiroho na kimaadili wakiwa bado gerezani.

"Tumebaini baadhi ya wafungwa wakitoka gerezani wanarudia makosa yaleyale na kujikuta wakirejea tena vifungoni. Tunaamini kwa kuwafikia kwa neno la Mungu na kuwajenga kimaadili, kutawasaidia kufanya maamuzi sahihi wanaporejea uraiani," amesema Shemkai.

Amesema lengo la mpango huo ni kuwahakikishia wafungwa kuwa Mungu yupo na anawapenda, ili baada ya kumaliza vifungo vyao waweze kurejea katika familia zao, kushiriki shughuli halali za kiuchumi na kuwa raia wema wenye mchango chanya kwa jamii, badala ya kurejea katika uhalifu.

Mbali na huduma za kiroho, Shemkai amesema umoja huo utaendelea kushirikiana na mamlaka husika kuhakikisha misaada inayotolewa inazingatia taratibu na inaleta tija kwa walengwa.

Viongozi wa Dini Washauriwa Kuwakaribia Waliotengwa

Kwa upande wake, Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Mailimoja Kibaha, Aaron Chuma amesema kudumisha upendo na amani katika jamii kunahitaji viongozi wa dini kuwa karibu na makundi yaliyotengwa, wakiwamo wafungwa, badala ya kuwabagua kutokana na makosa au mapungufu yao ya awali.

"Kuna wakati baadhi ya viongozi wa dini wanakataa kutoa huduma kwa watu waliokuwa hawahudhurii kanisa kwa muda mrefu, hata pale wanapohitaji faraja au msaada. Hili ni jambo lisilo sahihi na linahitaji mabadiliko ya mtazamo," amesema Chuma.

Ameongeza kuwa watu wote ni wa Mungu, hivyo viongozi wa kiroho wana wajibu wa kuwakumbatia waliotengwa, kusikiliza matatizo yao, kuwashauri na kuwaongoza katika kurejea kwenye maadili mema, huku wakiendeleza ujumbe wa amani, upendo na ushirikiano katika jamii.

Mmoja wa waumini waliohudhuria ibada hiyo, Nuru Samweli ameunga mkono mpango huo akisema utekelezaji wake utachangia kuimarisha upendo na amani nchini.

"Wafungwa muda mwingi huwa chini ya uangalizi wa askari magereza, lakini viongozi wa kiroho wanapowatembelea na kuwapa neno la Mungu, wanajisikia faraja na kurejeshewa utu wao," amesema.

Umoja wa Makanisa unaojumuisha Baraza la Kikristo Tanzania (CCT) na Jumuiya ya Makanisa ya Kikristo Tanzania (TEC), ulianzishwa kwa lengo la kuyaunganisha makanisa kushirikiana katika masuala ya kiroho, kijamii na kitaifa.

Kupitia umoja huo, makanisa yameendelea kutoa mchango katika kuimarisha amani, mshikamano wa kitaifa, maadili na kusaidia makundi yenye uhitaji, hatua inayosaidia pia juhudi za Serikali katika kudumisha utulivu na maendeleo ya jamii.

Tags: kuhudumiamakanisaWafungwaWajipanga
TNC

TNC

Next Post

Mbunge wa Mbarali kuvalia njuga migogoro ya mipaka

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company