Saturday, March 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Mwinyi ateuwa watano, wamo wastaafu

by TNC
December 22, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Unguja – Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi, ametangaza uteuzi wa wakurugenzi watano kuwa wenyeviti wa bodi mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ikiwemo wastaafu wawili.

Taarifa rasmi iliyotolewa leo Jumatatu, Desemba 22, 2025 na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Zena Ahmed Said, inaonyesha kuwa uteuzi huo unaanza rasmi leo.

Makame Hasnuu Makame, ambaye ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Meli na Uwakala Zanzibar (Shipco), ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usafiri Zanzibar (ZMA).

Sultan Said Suleiman, aliye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC), ameteuliwa kuongoza Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme la Zanzibar (Zeco).

Juma Burhani Mohamed, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA), atakuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA).

Dk Maudline Cyrus Castico, Waziri Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Zanzibar (Zawa).

Uteuzi huo pia unamshirikisha Dk Idrissa Muslim Hija, Katibu Mkuu Mstaafu wa SMZ, ambaye atakuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Karakana Zanzibar.

Tags: AteuwaMwinyiwamowastaafuWatano
TNC

TNC

Next Post

Tanzania and India sign agreement to advance traditional medicine

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company