Tuesday, December 16, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Wastaafu Dodoma kupatiwa vitambulisho vya kielektroniki

by TNC
December 16, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
0
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Wastaafu wa Dodoma Mjini Waagizwa Kuchukua Vitambulisho vya Kielektroniki

Dodoma – Wizara ya Fedha imetoa wito kwa wastaafu wa Wilaya ya Dodoma Mjini wanaolipwa na Hazina kufika Ofisi za Hazina Dodoma ili kupatiwa vitambulisho vya wastaafu vya kielektroniki.

Wito huo umetolewa na Mhasibu Mkuu kutoka Wizara ya Fedha, Jenipha Ntangeki, katika Ofisi ya Wizara ya Fedha, jijini Dodoma.

Ntangeki ametoa kauli hiyo wakati wa shughuli ya kutoa vitambulisho vya kielektroniki kwa wastaafu kutoka Wilaya ya Dodoma Mjini ambao wamefunguliwa dirisha hilo linalotarajia kudumu kwa siku 10.

Katika taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikali cha Wizara ya Fedha, mpango huo unalenga kuwatambua kikamilifu wastaafu na kuwarahisishia upatikanaji wa huduma bila usumbufu.

"Vitambulisho hivi ni tofauti na vya zamani ambavyo vilikuwa katika karatasi kwani utunzaji wake ulikuwa changamoto ndio maana tumekuja na hivi vya kielektroniki ambavyo ni imara na vitawawezesha wastaafu wetu kupata huduma bila changamoto kwa kuwa taarifa zao zitasomeka kwa urahisi," alisema Ntangeki.

Amesema vitambulisho hivyo vinafaa kwa matumizi rasmi hivyo wastaafu waliokabidhiwa wanaweza kuanza kuvitumia kupata huduma bila changamoto kutokana na kuwa ni vitambulisho vya kisasa na imara.

Akizungumza kwa niaba ya wastaafu waliofika Ofisi za Wizara ya Fedha kwa ajili ya kupata huduma hiyo, Andrew Makulukulu, amepongeza Serikali kwa kuendelea kuwajali hasa kwa kutambua shida wanazokutana nazo, hivyo wakaamua kuwapa huduma rahisi.

Wizara ya Fedha imeanzisha mpango huo wa ugawaji vitambulisho kwa wastaafu na wameanzia Wilaya ya Dodoma Mjini lakini wanaendelea nchi nzima kwa wastaafu wanaolipwa mafao yao na Hazina katika mikoa yote, mapema Januari 2026 kwa ratiba itakayotangazwa kupitia vyombo vya habari.

Tags: DodomakielektronikikupatiwaVitambulishovyawastaafu
TNC

TNC

Next Post

Tragedy as woman dies retrieving cash from fire

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company