Tuesday, December 16, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Wamiliki wa magari watakiwa kuwasikiliza madereva kudhibiti ajali

by TNC
December 15, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Wamiliki wa Magari Wasafirisha Abiria Watakiwa Kusikiliza Ushauri wa Madereva

Geita. Wamiliki wa magari yanayosafirisha abiria nchini wametakiwa kufuata ushauri wa madereva badala ya kuwaingilia kwa kuwapangia ratiba ngumu za safari, hali inayochangia ongezeko la ajali za barabarani.

Baadhi ya wamiliki wa magari hayo wamekuwa wakiwapangia madereva muda na idadi ya safari na fedha pasipo kufanya matengenezo ya vyombo vyao, hivyo kuhatarisha usalama wa abiria.

Kauli hiyo imetolewa Jumatatu Desemba 15, 2025 na Butasyo Mwambene, Ofisa Mnadhimu Kikosi cha Usalama Barabarani nchini wakati akizungumza na madereva na mawakala wa mabasi katika kituo kikuu cha mabasi Manispaa ya Geita.

"Wamiliki wa magari unapompangia muda yeye atapaa? Tuwasikilize madereva mnatoa maelekezo lakini magari hamtengenezi na hasa yanayotoka mjini kwenda vijijini, wamiliki msikilize dereva tusiangalie fedha tu," amesema Mwambene.

Onyo kwa Madereva Wanaopiga Muziki Usio na Maadili

Katika hatua nyingine, Mwambene ameonya baadhi ya madereva kupiga muziki usio na maadili.

"Kumbuka kwenye gari unakuta wanasafiri baba, mke na watoto, sasa mnaonyesha picha za utupu yale ni maadili ya Tanzania? Mnaenda msibani una wakwe mle ndani lakini vitu vinavyoonyeshwa ni aibu, wekeni vitu vya maadili mnatudhalilisha nchi," amesema.

Aidha, Mwambene amewataka mawakala kuacha kupandisha nauli msimu wa mwisho wa mwaka ambao umekuwa na abiria wengi, na kuwataka kuongozwa na hofu ya Mungu na kuridhika na kile wanachokipata.

Latra na Polisi Washirikiana Kudhibiti Usafiri

Naye Rajabu Selemani, Ofisa Mfawidhi kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra) Mkoa wa Geita amesema wamekuwa wakishirikiana na Jeshi la Polisi katika ukaguzi wa vyombo vya moto kudhibiti vilivyochakaa pamoja na madereva walevi, ili kupunguza ajali nchini.

Tags: AjaliKudhibitikuwasikilizamaderevaMagariwamilikiwatakiwa
TNC

TNC

Next Post

Zambia reaffirms commitment to Tanzania's transport and logistics sector

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company