Saturday, December 13, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Profesa azungumzia kukamatwa mhadhiri

by TNC
December 13, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
0
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Moshi. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, amesema taarifa za awali zinaonyesha mhadhiri wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) alikamatwa kutokana na matendo aliyofanya nje ya chuo.

Amesema hayo kutokana na taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuanzia Desemba 12, 2025 ikieleza mhadhiri wa UDOM amekamatwa chuoni akituhumiwa kwa uchochezi.

Taarifa hiyo iliyosambaa inaonyesha ni barua ya Jumuiya ya Wanataaluma ya Chuo Kikuu cha Dodoma (Udomasa) ya Desemba 12, 2025 ikipeleka ujumbe kwa wanachama wake.

Inaelezwa katika barua hiyo kuwa Desemba 9, mmoja wa wafanyakazi alikamatwa, nyumba yake ikafanyiwa upekuzi na akahojiwa kituo cha polisi kabla ya kuachiwa kwa dhamana.

Kwa mujibu wa barua hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Udomasa, Isaac Mahenge, mfanyakazi huyo ambaye hakutajwa jina alituhumiwa kutoa kauli katika mhadhara wa Desemba 8 (saa 4:30 asubuhi hadi 7:30 mchana) zilizodaiwa kuwachochea wanafunzi kushiriki maandamano ya Desemba 9.

Inadaiwa kauli hizo zilirekodiwa kwa siri na mtoa taarifa aliyekuwapo darasani na kutumwa kwa mamlaka za juu ambazo zilitoa agizo la kukamatwa kwake.

"Tukio hili linaashiria hali mpya ambapo mihadhara inaweza kuwa chini ya ufuatiliaji. Kwa sababu hiyo, tunawahimiza wote kuwa waangalifu mnapokuwa darasani, wakati sisi tukiendelea kuchunguza tukio hili na kubaini hatua zinazofaa kuchukuliwa," imeeleza barua hiyo ikiwataka kuwa makini.

Akizungumza na TNC Desemba 13, Profesa Mkenda amesema baada ya kuona taarifa hiyo ikizagaa mitandaoni, alifuatilia kwa mamlaka husika kujua ukweli, ambazo zimemweleza zinafuatiliwa.

"Hilo la mhadhiri kwamba amekamatwa kwa sababu ambazo zinatajwa huko ….nimeona kwenye mtandao inazunguka, nimeongea na Waziri wa Mambo ya Ndani, naye amesema analifuatilia japo kwa taarifa ya awali ni kwamba mhadhiri huyo atakuwa amekamatwa kwa sababu ya vitu alivyovifanya nje ya chuo siyo ndani ya chuo," amesema.

Profesa Mkenda amesema: "Kimsingi, wahadhiri wanapofundisha wana uhuru wa kufundisha lakini kwa kuzingatia weledi na maadili ya taaluma zao na siyo kwamba kuna mtu atapeleka polisi akae kwenye chumba aanze kumfuatilia akiwa anafunisha, kama mhadhiri anatoka nje ya mstari wa weledi au maadili ya kazi kuna hatua za kiutawala za kuchukua ndani ya vyuo."

Amesema kuna mkuu wa idara, makamu wa chuo, wakuu wa vitivo na seneti.

"Hatutarajii kabisa polisi watahusika kwa namna yoyote ile kwenda kusimamia namna ya kufundisha kwenye madarasa yetu, tutakuwa tumeenda mbali sana, hilo halipo," amesema na kuongeza:

"Wahadhiri tuna wajibu wa kufundisha kwa kuzingatia misingi ya kazi zetu, maadili na weledi. Sitarajii kwamba kutakuwa na usimamizi wa polisi kwenye kusimamia walimu wanapofundisha kwenye vyuo vikuu, endapo mhadhiri atakiuka maadili ya kazi yake, wapo wakuu wa vyuo na taratibu za kiutawala za vyuo zipo."

Tags: AzungumziakukamatwamhadhiriProfesa
TNC

TNC

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company