Saturday, December 13, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Mbunge Jenista Mhagama afariki dunia

by TNC
December 11, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
24
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Spika wa Bunge Atangaza Kifo cha Mbunge wa Peramiho

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu ametangaza kifo cha Mbunge wa Peramiho, Jenista Joakim Mhagama, kilichotokea leo Alhamisi Desemba 11, 2025, jijini Dodoma.

"Kwa masikitiko makubwa, naomba kutangaza kifo cha Mbunge wa Peramiho Mheshimiwa Jenista Mhagama kilichotokea leo 11 Desemba, 2025 jijini Dodoma. Natoa pole kwa waheshimiwa Wabunge wote, familia ya marehemu, ndugu, jamaa na wananchi wa Jimbo la Peramiho. Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu," ameeleza Spika Zungu kupitia taarifa rasmi.

Mhagama, aliyekuwa mbunge na kiongozi mwenye mchango mkubwa katika utumishi wa umma, alizaliwa Juni 23, 1967 na amehudumu katika nafasi mbalimbali ndani ya Serikali na Bunge la Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Bunge, mashirikiano yanafanyika kati ya Bunge na familia ya marehemu kuratibu taratibu za mazishi. Taarifa zaidi zitatolewa kadiri mipango itakavyokamilika.

"Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, amina," imeleza taarifa hiyo.

Tags: afarikiduniaJenistaMbungeMhagama
TNC

TNC

Next Post

Kizimbani kwa tuhuma za kuvamia, kuiba mali za Sh1.5 bilioni

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company