Friday, December 12, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Marufuku magari binafsi, bodaboda barabara za mwendokasi

by TNC
December 11, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

DART Yapiga Marufuku Vyombo Vyote Kutumia Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka

Dar es Salaam – Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) umepiga marufuku vyombo vyote vya moto isipokuwa mabasi ya ‘mwendokasi’ kutumia miundombinu ya mabasi yaendayo haraka kuanzia leo Jumatano, Desemba 10, 2025.

Marufuku hiyo imetangazwa leo Jumatano na DART kupitia taarifa kwa umma ya Kitengo cha Mawasiliano cha Uhusiano kwa Umma.

"DART inasisitiza vibali vyote vilivyowahi kutolewa vimesitishwa kuanzia Desemba 10, 2025," imeeleza taarifa hiyo na kuongeza:

"Doria na udhibiti vitaimarishwa ili kuhakikisha agizo hili linazingatiwa. Hatua za kisheria zitachukuliwa kwa yoyote atakayekiuka agizo hilo."

Marufuku hiyo imetangazwa kipindi ambacho kumekuwa na vyombo vya moto hususan magari ya Serikali na bodaboda kupita kwenye barabara hizo.

Novemba 25, 2025, Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega alitoa ruhusa kwa magari ya abiria kuanza kutumia barabara ya mwendokasi awamu ya tatu inayoanzia katikati ya jiji la Dar es Salaam kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere hadi Gongo la Mboto kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika barabara hiyo ya Nyerere.

Ulega alitoa ruhusa baada ya kukagua utekelezaji wa mradi huo ambao umekamilika kujengwa kwa asilimia 100 na kusisitiza umuhimu wa barabara hiyo kuendelea kutumika hadi hapo mtoa huduma kwa ajili ya kuleta mabasi katika barabara hiyo atapopatikana.

Tags: BarabarabinafsiBodabodaMagarimarufukuMwendokasi
TNC

TNC

Next Post

The rise and rupture: How two leaders' political alliance collapsed

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company