Sunday, December 14, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Kizimbani kwa tuhuma za kuvamia, kuiba mali za Sh1.5 bilioni

by TNC
December 11, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Dar es Salaam. Wakazi wawili wa Kinyerezi, Tumaini Moshi (33) na Gaspar Mmari (24) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu shtaka moja la unyang’anyi wa kutumia silaha na kujipatia vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh1.5 bilioni mali ya Klabu ya The Voice Tz Limited.

Washtakiwa hao wanadaiwa kabla ya kutekeleza wizi huo, waliwatishia watu kwa kutumia mawe, fimbo na nondo ili waweze kujipatia vitu hivyo bila kipingamizi.

Moshi na Mmari, pia wanakabiliwa na kesi nyingine ya uhaini mahakamani hapo, ambapo ipo katika hatua ya kutajwa.

Wamepandishwa kizimbani Desemba 11, 2025 na kusomewa shtaka lao na wakili wa Serikali, Frank Rimoy.

Wakili Rimoy ameieleza Mahakama kuwa washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya Jinai namba 28915 ya mwaka 2025 yenye shtaka moja la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Rimoy ameieleza mahakama hiyo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki na kisha kuwasomea mashtaka.

Akiwasomea hati ya mashtaka, Wakili Rimoy alidai Oktoba 29, 2025 eneo la Kinyerezi katika Klabu ya The Voice Tz Limited, washtakiwa kwa pamoja walifanya unyang’anyi wa kutumia silaha na kisha kuiba vitu vilivyokuwepo katika klabu hiyo.

Alidai kuwa siku hiyo ya tukio, Moshi na Mmari wanadaiwa kuiba viti 350 vya mbao na vya plastiki vikiwa na thamani ya Sh150 milioni.

Pia wanadaiwa kuiba vifaa vya ofisi vikiwa na thamani ya Sh40 milioni.

Iliendelea kudaiwa kuwa washtakiwa hao wanadaiwa kuiba runinga (TV) 57, zikiwa na thamani ya Sh480 milioni.

Washtakiwa hao pia wanadaiwa kuiba Music System wenye thamani ya Sh250 milioni na POS mashine ikiwa na thamani ya Sh80 milioni.

Mahakama iliendelea kuelezwa kuwa washtakiwa hao wanadaiwa kuiba vyombo vya jikoni vyenye thamani ya Sh25 milioni.

Vile vile, washtakiwa hao wanadaiwa kuiba vifaa vya baa yenye thamani ya Sh15 milioni.

Pia wanadaiwa kuiba vinywaji mbalimbali vyenye thamani ya Sh518 milioni, na kuiba fedha taslimu Sh16.9 milioni.

Mahakama ilielezwa kuwa jumla ya vitu hivyo vilivyoibiwa vina thamani ya Sh1.5 bilioni, mali ya Klabu ya The Voice Tz Limited.

Hata hivyo, kabla ya kutekeleza wizi huo, washtakiwa hao waliwatishia kuwapiga kwa kutumia mawe, fimbo na nondo, watu watatu ambao ni Jammy Galus, Masoud Ahmed na Benedict Katarunga ili waweze kupata vitu hivyo bila kikwazo.

Upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi haujakamilika na wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Baada ya kusomewa mashtaka yao, Hakimu Nyaki aliwaeleza washtakiwa kuwa shtaka linalowakabili halina dhamana kwa mujibu wa sheria, hivyo wataendelea kubaki mahabusu.

Baada ya kueleza hayo, aliahirisha kesi hadi Disemba 22, 2025 kwa ajili ya kutajwa na kuangalia iwapo upelelezi umekamilika.

Hii ni mara ya pili kwa washtakiwa hao kufikishwa Mahakamani hapo, kwani Novemba 7, 2025 walipandishwa kizimbani na wenzao 95 na kusomewa kesi ya uhaini.

Kesi hiyo ya uchunguzi wa awali (PI) namba 26540 ya mwaka 2025 inasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hassani Makube imepangwa kutajwa, Desemba 22, 2025.

Tags: BilionikizimbanikuibakuvamiakwaMaliSh1.5tuhuma
TNC

TNC

Next Post

Why families rely on year-end trips to strengthen unity

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company