Sunday, December 14, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

IGP, DPP kortini wakidaiwa kumshikilia waziri mstaafu kinyume cha sheria

by TNC
December 11, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Waziri Mstaafu Mwambe Afikishwa Mahakamani kwa Madai ya Kushikiliwa Kinyume na Sheria

Dar es Salaam. Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP) na wenzake wawiili akiwamo Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam (ZCO), wamefikishwa mahakamani kwa madai ya kumshikilia Waziri mstaafu, Geofrey Mwambe kinyume cha sheria.

Shauri la maombi namba 289778/2025 limefunguliwa na Mwambe akiwa mwombaji kupitia wakili wake, Hekima Mwasipu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Dar es Salaam, Kisutu Desemba 11, 2025 chini ya hati ya dharura.

Mwambe aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Mbunge wa Masasi, Mtwara (CCM), Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Waziri wa Viwanda na Biashara ameshikiliwa na Jeshi la Polisi tangu Desemba 7, 2025.

Maelezo ya Kukamatwa

Kwa mujibu wa hati ya kiapo inayounga mkono maombi hayo, Mwambe alikamatwa katika makazi yake eneo la Tegeta, usiku wa tarehe hiyo na watu waliojitambulisha kuwa maofisa wa polisi, akapelekwa Kituo cha Polisi Mbweni, alikohojiwa kwa tuhuma za uchochezi.

Baada ya hapo, alihamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi (Central) kwa usimamizi wa mjibu maombi wa tatu (ZCO) alikohojiwa mara ya pili kwa tuhuma za uchochezi kisha siku hiyo hiyo ya mahojiano alipelekwa mahabusu katika Kituo cha Polisi Kigamboni.

Kutokana na hali hiyo, wakili wake Mwasipu kwa niaba yake, amefungua shauri hilo dhidi ya IGP, DPP na ZCO, akiiomba Mahakama iamuru Mwambe afikishwe mahakamani na apewe dhamana kwa masharti yatakayowekwa na Mahakama hiyo.

Maelezo ya Wakili

Wakili Hekima Mwasipu amesema wamefungua maombi hayo mahakamani kwa kuwa Mwambe ameshikiliwa kinyume cha sheria bila kupewa dhamana kwa makosa yanayodhaminika.

"Pale kosa analotuhumiwa mtu anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi linapokuwa na dhamana, lakini polisi au wanaomshikilia wanakuwa hawataki kutoa dhamana basi unaweza kupeleka maombi kama haya katika Mahakama ya Wilaya au Mahakama ya Hakimu Mkazi kuomba huyo anayeshikiliwa apewe dhamana na Mahakama," amesema Mwasipu.

"Utaratibu wa kisheria ni kwamba, mtu anapokamatwa anapaswa kufikikishwa mahakamani ndani ya saa 24 lakini mpaka leo hajapelekwa mahakamani."

Tarehe ya Kusikilizwa

Maombi hayo yamepangwa kusikilizwa Jumatatu, Desemba 15, 2025 saa 3:00 asubuhi na Hakimu Mkazi Mkuu, Hassan Makube.

Mwasipu amesema alifahamishwa na familia ya Mwambe, kisha alikwenda kuzungumza naye uso kwa uso katika Kituo cha Polisi Kigamboni alikopelwa baada ya kukamatwa kwa tuhuma za uchochezi.

Amesema alifanya mashauriano na wanaomshikilia kwa ajili ya dhamana, lakini haikuwezekana na wanaendelea kumshikilia, ndio maana wameamua kuchukua njia za kisheria ili apate haki yake ya Kikatiba ya kuwa huru.

Mwambe Ahamishwa Kituo Kingine

Hata hivyo, wakili Mwasipu amesema inadaiwa kuwa Mwambe amehamishwa kutoka katika Kituo cha Polisi Kigamboni alikokuwa anashikiliwa na hawajui amepelekwa wapi.

"Leo asubuhi familia ilimpelekea chakula wakaambiwa kuwa hayupo wameshamtoa, sasa mpaka sasa hivi hatujui yuko katika kituo gani cha polisi. Tunazidi kufuatilia pamoja na familia ili kujua amepelekwa kituo gani cha polisi," amesema wakili Mwasipu.

Wakili Mwasipu amesema wanaendelea kufuatilia ni kwa nini mpaka sasa anashikiliwa kwa kuwa, kama kulikuwa na sababu za kuendelea kumshikilia zaidi ya muda huo, utaratibu wa kisheria unawataka waombe ruhusa mahakamani.

"Lakini hilo halijafanyika. Sasa tunafuatilia kukutana nao (polisi) watuambie ni kwa nini ni zaidi ya saa 24 bado anashikiliwa ili haki yake ya kuwa huru iweze kupatikana," amesisitiza wakili Mwasipu.

Tags: chaDPPIGPKinyumekortiniKumshikiliamstaafusheriawakidaiwaWaziri
TNC

TNC

Next Post

University Vice Chancellor warns excessive AI use undermines students' critical thinking

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company