Sunday, December 14, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Watalii waongezeka Zanzibar mwezi wa kumi na moja, wageni kutoka Italia wapo mbele

by TNC
December 10, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Zanzibar Yapokea Watalii 72,833 Mwezi Novemba 2025

Unguja – Takwimu mpya zinaonesha kuwa Zanzibar ilipokea watalii wa kimataifa 72,833 katika kipindi cha Novemba 2025, ikiwa ni ongezeko la asilimia 8.6 ikilinganishwa na wageni 67,049 waliowasili kipindi kama hicho mwaka 2024.

Taarifa kutoka Tume ya Utalii Zanzibar kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali zilizotolewa Desemba 8, 2025 zinaonyesha mwenendo huu.

Hata hivyo, takwimu hizo zinaonyesha kupungua kwa asilimia 16 kutoka wasafiri 86,740 waliowasili Oktoba 2025, hali inayodhihirisha mzunguko wa misimu ya utalii visiwani wakati kilele cha msimu wa juu kikianza kupungua.

Ulaya Iendelea Kutawala Soko la Utalii

Wasafiri kutoka Ulaya waliendelea kutawala soko, wakiweka asilimia 73.1 ya wote waliowasili Novemba. Italia iliongoza kwa asilimia 12.2 ya wageni wote, ikifuatiwa na Ujerumani (asilimia 7.7) na Ufaransa (asilimia 7.4), huku Japan ikiwa na idadi ndogo zaidi ya asilimia 0.1.

Masoko yanayochipukia ikiwemo Poland, India, Urusi, Israel, China na Ukraine yalionesha kupungua kidogo kwa asilimia 1.1 ikilinganishwa na takwimu za Oktoba.

Usafiri wa Anga Njia Kuu ya Kuingia

Usafiri wa anga uliendelea kuwa njia kuu ya watalii kuingia Zanzibar, kwa asilimia 93.7 ya wote waliowasili kupitia uwanja wa ndege Novemba. Kati ya hao, abiria 54,263 waliwasili kwa ndege za kimataifa, huku 13,960 wakitua kwa safari za ndani ya nchi.

Kwa upande mwingine, wasafiri 4,610 pekee waliingia visiwani kwa njia ya bahari, ambapo wanne tu walikuwa watalii waliowasili kwa meli kubwa za kitalii.

Mapumziko Lengo Kuu la Watalii

Wasafiri wa likizo waliendelea kuipa nguvu sekta ya utalii, huku watalii 72,433 (asilimia 99.5) wakitembelea visiwa hivyo kwa madhumuni ya mapumziko. Ni asilimia 0.4 tu waliokwenda kuwatembelea ndugu na jamaa, huku asilimia 0.1 wakiwasili kwa sababu nyinginezo.

Takwimu za Rika na Muda wa Kukaa

Kwa upande wa rika, wenye umri kati ya miaka 15–64 walichangia sehemu kubwa ya watalii waliowasili visiwani kwa asilimia 87.7, wakifuatiwa wazee (miaka 65 na kuendelea) kwa asilimia 8.2, na watoto kwa asilimia 4.1.

Jumla ya vitanda 884,430 vilikuwa vinapatikana mwezi huo, huku 601,266 vikiuzwa, sawa na asilimia 68 ya matumizi.

Kuhusu muda wa kukaa, taarifa inaonyesha kuwa watalii hao walikaa wastani wa siku nane, ambapo asilimia 32.8 walichagua kukaa kwa muda wa wiki moja.

Tags: ItaliakumikutokaMbeleMojaMweziwageniwaongezekawapoWataliiZanzibar
TNC

TNC

Next Post

Tanzania demands diversified climate finance as philanthropy steps in to close Africa's funding gap at global environmental assembly

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company