Saturday, December 13, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Mashauri 15 ya Wazalendo yatajwa mahakamani leo

by TNC
December 10, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Unguja – Mashauri 15 kati ya 17 ya Unguja yametajwa katika Mahakama Kuu ya Zanzibar yanayopinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29, mwaka huu huku mashauri mawili ya Jimbo la Makunduchi na Kiembesamaki kutajwa kati ya Desemba 14 au 15.

Mashauri hayo yamefunguliwa na wanachama 15 wa Chama cha ACT Wazalendo na waliokuwa wagombea wa nafasi za ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kwenye uchaguzi Mkuu dhidi ya wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo 15 na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.

TNC imebaini kuwa mashauri hayo yametajwa Jumanne Desemba 10, 2025 mbele ya Naibu Mrajisi Faraji Shomar Juma katika Mahakama hiyo iliyopo Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja.

Akitoa maombi mahakamani, Wakili kutoka upande wa walalamikaji, Rajab Abdallah Rajab wameiomba mahakama kupitia majibu ya mashauri yaliyoletwa upande wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, kwani mashauri hayo yalikuja asubuhi kwa ajili ya kutajwa.

Hivyo, hawajapata nafasi ya kuyapitia majibu hayo kwa lengo la kuendelea na mambo mengine ya kisheria mahakamani hapo.

Kabla Mahakama kuridhia ombi hilo, Wakili kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mbarouk Suleiman Othman alikubali kutoa majibu hayo na kutoa angalizo, kuwa majibu hayo yasitumike kupitia pingamizi ambazo tayari zimewasilishwa katika utetezi wao.

"Mheshimiwa Naibu Mrajisi, Sisi hatuna tatizo na kupewa majibu hayo lakini tunaomba wasije wakayatumia kupitia pingamizi tulizowasilisha," amesema Mbarouk.

Akitoa ufafanuzi wa hilo, Wakili Rajab amesema wanachohitaji ni kupitia majibu ya Serikali ili kutoa majibu yao (walalamikaji) ndipo mashauri yaendelee.

Hivyo, Mahakama imejiridhisha kuwa upande wa wajibu na wamekabidhiwa nyaraka za kufungulia kesi kwa mujibu wa sheria.

Pia, Mahakama imeagiza kuwa walete maombi ili kupatiwa nakala za majibu hayo yaliyowasilishwa na wajibu maombi pamoja na hati za kiapo kinzani.

Kwa hivyo, Naibu Mrajisi ameahirisha mashauri hayo hadi Desemba 18, 2025 saa 3:00 asubuhi kwa ajili ya kutajwa tena.

Naibu Mrajisi amesema katika tarehe hiyo, walalamikaji wataitaarifu mahakama kama wanakusudia kuwasilisha majibu kwa majibu yalioletwa ya wajibu maombi au hatua nyengine za kimahakama zinaweza kuendelea ikiwemo kesi hiyo kupangiwa Jaji.

Akizungumza nje ya Mahakama, Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho, Omar Said Shaaban amesema timu yao ya mawakili inazingatia ratiba na taratibu zote zilizowekwa na Mahakama.

"Hadi kufikia sasa tunaridhishwa na hatua zinazoendelea na tunatumia muda huu wa kuahirishwa kwa mashauri kujiandaa kwa hatua zinazofuata za kisheria," amesema Omar.

Ameeleza kuwa, kwa kuwa mashauri hayo yapo rasmi mikononi mwa mahakama, hawatatoa maoni kuhusu ushahidi au kiini cha kesi kwenye vyombo vya habari hivyo wameomba wananchi kuheshimu utaratibu wa sheria.

Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29, Chama hicho kilishinda majimbo 10 na Chama cha Mapinduzi (CCM) kikishinda majimbo 40 kati ya 50 yaliyopo Zanzibar.

Chama hicho kilifungua mashauri 25 ya kupinga matokeo hayo, 17 Unguja na nane Pemba huku mashauri mawili ya jimbo la Makunduchi na Kiembesamaki kutajwa kati ya Desemba 14 au 15.

Majimbo ambayo wameyafungulia kesi ni Malindi, Amani, Nungwi, Kijini, Bumbwini, Chaani, Mpendae, Kiembesamaki, MwanaKwerekwe, Tumbatu, Makunduchi, Pangawe, Chumbuni, Mwera, Mtoni, Welezo na Kikwajuni.

Tags: leomahakamanimashauriWazalendoyatajwa
TNC

TNC

Next Post

What Tanzania expects at international meeting as global environmental decisions take shape

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company